Na Jasper “Kido” (@KidoJapa)
Salaam wandugu
Wadogo nanyi wakuu,
Ishikeni hii salamu
Pamoja na ujumbe huu,
Imenifika kalamu
Nasaha hizi nipate nukuu,
Yapo mengi muhimu
Ya kuandika nyingi juzuu,
Majanga yametusibu
Ye hajali, yuko majuu,
Sokoni kenda kuzuru
Kuwadi aliyekubuu,
Afisa miradi bubu
Msafiri asiye miguu,
Tunalo tatizo sugu
Matonya ana nafuu,
Sharti kitune kibubu
Ndo sera na ilani adhimu,
Si mtamu mkono mtupu
Wa asali ni wenye marupu,
Mtu hashibi utu
Wala nasaha zae Butiku,
Bali ni kwa mlo tu ulosadifu
Nd’o njaa ‘tatoka mkuku,
Hivyo twavikwa jukumu
Mgeni kumkarimu,
Ajapo aleta karamu
Naye twapaswa mheshimu,
Mpaka ndani mgeni karibu,
Tena ujisikie huru,
Uungwana kumsujudu
Hata tukifanywa kibudu,
Kwako ewe kapuku
Kamwe sijethubutu,
Ukome na ni marufuku
Mgeni kosea nidhamu,
Nawe msomi mwenye mabuku
Kuhoji sifikiri katu
Bali sifu na kuabudu
Ugeni uloshika hatamu.
Comments are closed.
Chunga ewe umbu wangu
Sijeleta msiba kwangu
Kayani ukatujazia utungu
Yakupasani kulivunja jungu?
Wanene wenye misuli
Weye tulia tuli
Chunga kutojijali
Kabla haijaja ajali
Vipenziwe makatili
Si simile majahili
Kibaini yako methali
Shingoyo taichinjia mbali.
Hala Hala ujihadhari
Yakikufika utatahayari
Usizuzuliwe na hariri
Moyo huzificha Siri.
Si tisho hili shauri
Wende pole ninashauri
Lau uitaraji shubiri
Hekima kutahadhari
Mbona hujibu mapigo ya Muhemsi, au amepiga kwenye mshono
Ndio nyie mko hapa kushadadia uhuru wa moni ya wananchi
Huku mnafuta comment za wengine kama haziwafurahishi…
Kwani nimetukana?
Useless bogus blog
A show off sort of…bollocks