Mwaliko wa Kuchangia katika Antholojia ya
Simulizi za Kufutwa na Kurejesha: Kilichojificha Nyuma ya Midahalo ya Kianazuoni ya Miaka ya 1970.
Uhenga Collective inawaalika waandishi, wasomi, wasanii, washairi, watafiti, na watendaji wa tamaduni kuchangia makala katika antholojia ya lugha nyingi na tanzu mbalimbali inayohaririwa na Demere Kitunga, Diana Kamara na Rehema Chachage. Antholojia hii inarejelea na kufakari Midahalo ya Kifikra ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam ya miaka ya 1970—na athari zake za baadaye kwenye: mitazamo ya kuondokana na ukoloni mamboleo, ukombozi wa wanawake kimapinduzi, mwingiliano wa mifumo kandamizi kama tabaka, rangi, nasaba nk.Antholojia inalenga kuangazia historia za wanawake zilizofutwa, zilizonyamazishwa, na zilizotengwa katika maisha ya wanajamii ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam: wanafunzi, wahadhiri, wanaharakati, wasanii, wanafunzi wa na walhadhiri wa kimataifa na washirika wao—ambao kazi yao ya kifikra na mapambano yao ya kila siku hayajapewa nafasi katika simulizi kuu. Tunakaribisha kazi ambazo zinachunguza kwa kina, kwa ubunifu na kwa upana historia za kijamii na za kifikra za Chuo Kikuu, zinazoangazia mienendo ya kijinsia katika uzalishaji wa maarifa, na kuleta simulizi, uchambuzi na kazi za sanaa zinazopinga ukimya uliopo katika historia inayotawala.Tunatafuta kazi zitakazojenga uwanda mpana wa namna historia hii inavyokumbukwa, zinazotikisa hadithi za kiume zilizotukuzwa, na zinazowazia upya misingi ya ukombozi kwa vizazi vijavyo.


Leave A Comment