SIKU YASHAFI ADAM SHAFI
Umewahi kusoma kazi yoyote kati ya hizi?
“Kasri ya Mwinyi Fuad”
“Kuli”
“Vuta Nkuvute”
“Haini”
“Mbali na Nyumbani”
Baada ya kuzisoma, umewahi kuwa na hamu ya kukutana, kubadilishana mawazo na kujadiliana na mwandishi wake?
Taasisi ya “Kitabu kwa Maendeleo Tanzania (KMT)” kwa kushirikiana na “Soma Book Café” inawaletea “Siku ya Shafi Adam Shafi”. Washiriki wa siku hii watapata nafasi ya kuzijadili kazi za mwandishi huyu nguli wa fasihi na kubadilishana naye mawazo na uzoefu.
Mjadala utafanyika siku ya tarehe 5/9/2015 kwenye Mkahawa wa Soma (Soma Book Café)
Kwa maelezo zaidi juu ya mjadala huu piga: 0653619906 (Ado) au 0712568699 (Jasper)
KITABU NI SILAHA
KITABU KINA RAHA!
__._





