Salim Khatri:
Ukiweka
mazingira mazuri kwa wawekezaji utaambiwa unakumbatia wageni. Prof. Muhongo
alipowaambia wakina Mengi walipe $700,000 kwa ajili ya tender document na
$3,500,000 for data ili wakashindane na wenzao kupata vitalu vya mafuta na
gesi, wakamwambia hana uzalendo.
Emmanuel Sulle:
[Salim] kwa sentensi yako hii
ni kweli Muhongo hana uzalendo kwa sababu hata hao wawekezaji wa nje unawaosema
wengi wanapewa misaada au mikopo nafuu sana kutoka nchi zao kulinganisha na
hapa kwetu. Je, una habari hii?
Nchi yoyote inaweza kuendelea
kwa kuwaendeleza watu wake na siyo kuwaleta wageni ambao faida wanakwenda
kuziwekeza nchini mwao. Fanya utafiti kwenye sekta ya madini, tumepoteza hela
kiasi gani.
Chambi Chachage:
Nimewahi
kumuuliza mtafiti mmoja wa masuala ya gesi na mafuta ambaye hana mapenzi
na Muhongo kwamba: Hivi tukiweka pembeni huo ‘ujuvi’ na ‘majigambo’ ya Profesa,
je, ni kweli hatuna watu wenye uwezo wa kuwekeza kwenye gesi? Akanijibu:
HAKUNA! Nikamuuliza hata kina Bhakresa, Mengi, Rostam et al. wakijikusanya?
Akasema: Hata iwe hivyo hawana mtaji wa kutosha kutafuta na kuchimba
gesi/mafuta. Katika hili Muhongo ni ‘mwongo’ pia?
Juma Mwapachu:
Huu
ni uelewa hafifu kabisa kuhusu suala la uwekezaji kijumla hata kama ni kuhusu
sectors ambazo wengi wetu wanadhani mitaji ya uwekezaji inatoka katika mifuko
ya watu binafsi. Hakuna matajiri binafsi wanaowekeza katika sectors hizi kwa
kutumia fedha zao. Mitaji inatokana na proofs za kuweko dalili nzuri za kuwepo
rasilimali. Fedha zipo nyingi katika global capital markets. Tatizo ni Serikali
zetu kutokuwa na confidence na watu wenyewe na kuwa tayari kukubali mabilionea
kuibuka. Tuondokane na fikra hizi zisizo na manufaa. Tubadilike la
sivyo tutabaki nyuma.
Emmanuel Sulle:
Huh!
I
am not sure if this researcher is really saying the truth! It is not true that
we need cash like that. Govt can issue loans to its committed citizens or
companies to do business. This is how some countries have done either in Asia
or Europe. And, govt too can seek loans from financial institutions to
subsidize the locals business!
There
are also different models in which locals can participate in this business and
that is joint ventures. In Asia, people owns wells of oils simply because they
did not give out their oil/gas land but rather invited investors to harvest
while paying them royalties/certain amount of revenues in special/specific
agreement(s).
[…]
Excellent
point from Hon. Mwapachu.
If
we “wanazuoni” still think that we as “a country” are so
poor then we are not different from “laymen”, excuse my language, but
that is the reality. The national wealth is not simply pegged on the revenues
you see/count. Infact, the value of our nation increased several folds in the
global capital from the day we discovered gas, Tanzanite etc. Unfortunately, we
are here because of our choices, and because of these choices, we are likely to
continue to be here unless we change our mindset and make better choices
[…]
Tukiuchukulia
huu mjadala kama mapambano kati ya Mengi na Muhongo tutakuwa tunakosea. Muhongo
ni waziri, ni mtumishi wa umma. Anawasilisha maoni ya serikali tuliyoiweka
madarakani. Kwahiyo, yeyote anayehoji hoja zake anafanya vile kwa mujibu wa
haki zake kama mwananchi (mwenye nchi) na asingeweza kujibiwa kwa dharau kama
alivyofanya Muhongo.
Pili,
suala la wazawa kupendelewa, ni dhana inayotumika duniani kote kulinda maslahi
ya nchi na watu wake. Anayeona hili nalo mbaya hajui msingi wa hili jambo.
Katika nchi karibu zote za Ulaya na America, wazalishaji wa ndani wanapewa
ruzuku wazalishe kwa ajili ya mauzo ya nje au ndani ili kuustawisha uchumi wa
nchi zao. Labda sisi tunaona wivu watanzania wenzetu wakiendelea, kwahiyo bora
wageni waje waendelee.
[…]
Chambi Chachage:
Mkopo
watoe vipi/wapi kama hadi leo tunaambiwa hata mabilioni ya kuwalipa watu RUIPA
hawajayatoa? Kwenye ‘Escrow’? Wauze ‘Sovereign Bond’? Wakope ‘World Bank’ na
‘IMF’? Hebu tufanya mahesabu. Njia rahisi ni kutaja kiwango cha fedha ambacho
Serikali inacho (kwa mfano, bajeti ya nchi ni trilioni ngapi sasa?) na
kukilinganisha na hizo zinazosemwa ni gharama (halisi) za kutafuta na kuchimba
gesi/mafuta. Nakisi ni hasi, chanya? Waipe TPDC?
PS.
Halafu tukumbuke kwamba wanaochangia kufadhili bajeti yetu ndio hao hao ambao
makampuni ya nchi zao yanatafuta gesi na mafuta nchini kwetu – rejea ramani ya
utafutaji wa gesi/mafuta iliyopo kwenye tovuti ya TPDC.
Alex Kobalyenda:
Exactly
my Point Comrade…
We put our emotions and political fronts too high and ignore uhalisia wa mambo.
If we can’t feed ourselves, who will agree tukope to gamble?
It’s sad but ndio ukweli wenyewe….best option ndio hiyo kuvizia wapate then
we jump wagon…..with good policies in favor ta Mtanzania.
Salim Khatri:
And
that’s why Prof. Muhongo gets attacked from all sides for stating facts that
are common knowledge in the oil and gas industry.
[…]
[…]
Hizo dharau zinatokea wapi? Yaani kuambiwa mkashindane kutengeneza
juisi, biashara mliyokuwa na ujuzi pamoja na uzoefu nao ndiyo dharau? Mbona ni
ukweli mtupu? Bakhressa, Muhammed Enterprise, Mengi (matajiri watatu wakubwa
kabisa nchini) biashara wanayoshindana ni kutengeneza maji, soda na juisi. Huo
ndiyo ukweli kaka. Sasa na mimi kaniweke kwenye hilo kundi la watu
wanaoshindana kutengeneza juisi kama nitakuona unanidharau ama unanipandisha
chati.
Kupewa ruzuku uendelee kuzalisha ili ulinde ajira za nchini siyo sawa
na kukabidhiwa bure biashara usiyokuwa na ujuzi wala uzoefu nao. Mfano
uliotolewa na Prof. Muhongo ndiyo huo wa Mengi kukabidhiwa leseni za madini
zenye ukubwa saw ana Dar es salaam tatu. Mpaka leo kazalisha madini kiasi gani?
Akataka akabidhiwe hoteli ya Kilimanjaro kwa bei chee wakamkatalia kumpa
upendeleo huo. Baada ya kuikosa Hoteli ya Kilimanjaro keshajenga hoteli ngapi
mpaka hivi sasa? Alichotaka Mengi apewe hoteli kwa USD 1 million (ndiyo
lilikuwa dau lake – the lowest bidder) halafu akaiuze kwa mtu mwengine for USD
15 million na kuweka mfukoni USD 14 million net profit. Hapo mgonjwa anayesugua
benchi kwenye hospitali ya Mwananyamala anafaidika vipi?
[…]
Bado
sioni wapi Prof. Muhongo ameleta hadithi…
Mavere Tukai:
Utaona
vipi wakati umeamua kuwa na selective blindness Nd. Salim??
Sabatho Nyamsenda:
Hili jukwaa nadhani linaionea wivu JF na linataka kuiiga. Muda si mrefu
tutaenda kulekule. Nashauri tujikite zaidi katika hoja badala ya mashambulizi
ya watu binafsi ili tuwe na uwezo wa kuchambua.
Suala hapa ni umiliki, udhibiti na ufaidikaji wa rasilimali. Nani
amiliki, na kwa faida ya nani?
Kuna lugha mbili zinazotumika: “watanzania” na “wazawa”. Hizi ni
tofauti kabisa.
Kuna mtu kashadadia hoja ya “wazawa” na kusema kuwa duniani kote ndivyo
ilivyo. Pengine hatujaingia zaidi katika historia ya “uzawa” hapa nchini, na
kwingineko. Yapaswa turejee mjadala wa uraia katika baraza la sheria la
Tanganyika mwaka 1960, ambako hoja ya “uzawa” ilikuwa ikitumika kudai haki ya
uraia, na haki ya utawala kwa watu weusi tu. Nyerere aliipinga na
kutishia kujiuzuru uwaziri mkuu. Hoja hiyo ilijitokeza tena wakati wa
ubinafsishaji ambapo wazawa walidai kupendelewa. Mwalimu aliipinga kwa nguvu na
kuiita “ukaburu” rejea hotuba yake Kilimanjaro Hotel, mwaka 1995.
Hoja hii ilipoibuliwa na akina Mengi wakati wa gesi, “mzawa” ni nani
hasa? Katika “wazawa” Bakhresa, Manji na Rostam wamo? Katika kile kisa cha
Kongamano la Udasa nilichokisimulia hapo awali, Muhongo alitaja watanzania 10
walioohodhi umiliki katika madini. Mengi alikuwa wa tatu. Wakati akitaja majina
mawili ya mwanzo, japo ni Watanzania, majina yao yanaonyesha dhahiri kuwa wana
asili ya Kiasia. Washiriki katika Ukumbi wa Nkrumah walikuwa wakipiga kelele
“sio wazawa hao”!
Kwa hiyo watetezi wa uzawa kueni macho, na mseme waziwazi kinachotetewa
ni nini? Dhana ya Uzawa imeshatafitiwa vya kutosha (rejea vitabu vya Mamdani 1.
Citizen and Subject; 2. When Victims become Killers; 3. Define and Rule), na
imeonekana kuwa chanzo cha migogoro mikubwa ya kisiasa pale ambapo “wazawa”
wanahisi kunyang’anywa haki zao na “wahamiaji”. Mfano wake ni mauaji ya kimbari
ya Rwanda.
Hilo mosi. Pili, tunaposema “Watanzania wamiliki” tunamaanisha nini
hasa? Hapa kuna watetezi wa mabepari wa bongo (akina Mwapachu); watetezi wa
umiliki wa dola kwa niaba ya Watanzania; na watetezi wa mchanyato (dola +
binafsi). Tungejikita katika kujadili njia hizi na kuonyesha ni ipi yenye tija
na manufaa kwa sasa na vizazi vijavyo.
Kwa vyovyote vile, hapa nchini hakuna tabaka la mabepari wenye mtaji
(national bourgeosie) bali tuna tabaka la mawakala (compradorial bourgeosie).
Uwekezaji mkubwa binafsi wa ndani utahitaji tulijenge tabaka hilo, kwa
kulipatia upendeleo na kuliruhusu kupora pale inapowezekana. Tufumbie macho
Escrow, EPA, Richmond, ukwepaji kodi n.k., na tuwahimize hao waporao kuwekeza
fedha “zao” katika shughuli za uzalishaji. Ndivyo zilivyofanya nchi zote
zilizojenga tabaka la mabepari wa ndani, zikiwemo Japan na Malaysia. Ndiyo
maana ya upendeleo kwa “wazawa” hiyo!
Chambi Chachage:
Salim,
ungekuwa wewe unaambiwa maneno hayo hapo chini ungejisikiaje ilhali unajiona ni
mzalendo/mzawa?
Mheshimiwa
Spika, gesi asilia na mafuta: Napenda kurudia tena hakuna Mtanzania aliyezuiwa,
hayupo wala hatujamzuia Mtanzania yeye akatafute kampuni waje naye akiwa na
ubia hatujazuia, na tuna kampuni ya Watanzania ambayo tayari inafanya kazi na
Wa-Australia na wote hata wao wenye kampuni hiyo walikiri kwamba hawana fedha,
hawana teknolojia ndiyo maana wametafuta kampuni ya Australia wafanye nayo
kazi.
Kwa
hiyo ndugu zangu kama nia ya mtu ni kitalu, wewe njoo na wawekezaji mshindane.
Lakini nataka kusisitiza tena haitatokea kwamba kuna mtu atapewa kitalu yeye na
familia yake, haiwezekani! Na hii hata mtu aandike asubuhi na mchana, aimbe,
haiwezekani! TPDC ndiye anayetuwakilisha, anawakilisha Watanzania wote tajiri
na maskini, lakini hamna vitalu vya familia hapa.
Mheshimiwa
Spika, sheria ambayo tunayoileta na nimeshaongea na wakuu wangu wote kwamba hii
gesi iliyogundulika tusipokuwa waangalifu tunaweza tusifaidike. Ndiyo maana ni
lazima tuwe waangalifu kwa sababu huyu mtu akivuna gesi, sasa tuamue je, hizo
fedha kama kitalu ni chake ni fedha zake na familia yake, lakini kama ni za
TPDC ni zetu wote, za Watanzania wote.
Kwa
hiyo msidanganywe na hadithi yoyote na tutakuja hapa, sheria tunayoileta hapa
ya sovereign fund ni kwamba zile fedha hata Hazina hawatazichukua zile fedha
kwamba yamepatikana mabilioni tunaenda tunayamwaga yote pale Hazina, hakuna
kitu kama hicho. Patatengenezwa mfuko maalum na fedha zile hazitatoka bila ya
uthibitisho wa Bunge.
Kwa
hiyo Rais, Makamu wa Rais, Waziri Mkuu hakuna atakayetoa ruhusa kwenda kuchukua
zile fedha, lazima Bunge litoe idhini. Kwa sababu hawa Wabunge ndiyo
wanaowawakilisha wananchi. Tutaweka kwamba haziwezi kutolewa
zote zig zag, itakuwa ni kwa percent kwa sababu sisi wenyewe tunajua ukimpa mtu
hapa shilingi milioni mia moja ukasema tumia tuletee mrejesho ataonesha
amezimaliza zote milioni mia moja.
Kwa
hiyo hatuwezi kufanya kosa kama hilo, itakuwa ni percent fulani kwa mwaka
kusaidia bajeti kwa mwaka huo, fedha zingine zinatunzwa kwa ajili ya vizazi
vinavyokuja na kusaidia uchumi wa nchi utengemae, na ndiyo maana kama
tunakuwa na sovereign fund ni hatari sana kuruhusu mtu na familia yake awe na
kitalu. Haya yote ndiyo nilikuwa nataka ayaweke kwenye bajeti, sasa yakawa ni
hadithi tu.
– PROF. MUHONGO – UKURASA WA 311 –
312 WA HANSARD YA MAJADILIANO YA BUNGE YA 30 MEI 2014
Zitto Kabwe:
Jambo
usilolijua ni sawa na usiku wa kiza. Hiyo hadithi hapo [juu] bado ni hadithi
tu.
Emmanuel Sulle:
Mh
Zitto, tusaidie, hadithi ipi unayoizungumzia? ya Muhongo?
Salim Khatri:
Nilikuwa
nataka kuuliza hicho hicho. Kipi kwenye maneno aliyonukuliwa Prof. Muhongo ni
“hadithi”, yaani masimulizi yasiyokuwa na ukweli.
Jambo
usilolijua ni kweli giza na ndiyo maana Prof. Muhongo anasema anapozungumzia
hayo mambo uchukue karatasi na kalamu.
Chambi Chachage:
Labda
wasiokuwa katika “usiku wa kiza”, i.e., wanaojua “jambo” ni
wenye hoja hii aliyokuwa anaijibu kwa “hadithi”:
Mheshimiwa
Spika, katika bunge la bajeti
kwa mwaka wa fedha 2013/2014, kambi ya upinzani bungeni iliitaka serikali
kuhakikisha wananchi wa Tanzania wanamiliki na kunufaika na rasilimali za Taifa
hili ikiwa ni pamoja na gesi iliyogunduliwa katika mikoa ya Lindi na Mtwara.
Aidha miezi michache baadaye Tanzania ilishuhudia mivutano mikubwa kuhusu
uwekezaji katika sekta ya gesi hapa nchini. Mvutano huo ulijitokeza
kati ya taasisi ya Uwekezaji nchini (TPSF), kupitia kwa mwenyekiti wa taasisi
hiyo na serikali kupiti kwa Waziri mwenye dhamana ya Nishati na Madini kuhusu
taasisi hiyo (TPSF) kuwekeza katika suala la gesi nchini.
Mheshimiwa
Spika, katika maoni yake, TPSF
ilisisitiza umuhimu wa ushirikishwaji wa Watanzania katika uchumi wa gesi na
kuishauri serikali kusitisha ugawaji wa vitalu vya gesi hadi sera ya gesi itakapokuwa
tayari na taasisi hiyo iliomba kukutana na Waziri Muhongo mwenye dhamana ya
nishati na madini kwa majadiliano zaidi. Tofauti na ilivyokusudiwa, serikali
ilijibu kupitia vyombo vya habari kwamba mpango wa kugawa vitalu vya gesi na
kuingia mikataba uko palepale kama ulivyopangwa kufanyika bila kuzingatia
mchango ambao ungetolewa na taasisi ya uwekezaji hapa nchini. Mbaya zaidi
serikali ilikataa bila kumng’unya maneno kwamba haina mpango wa kukutana na
TPSF, kwani kufanya hivyo ni kupoteza muda, na kuongeza kuwa uwezo wa
wafanyabiashara wa Tanzania ni kuwekeza kwenye soda na juisi, si kwenye sekta
ya gesi. Septemba 7, mwaka 2013, mtu aliyejitambulisha kwa jina la “CCM
Tanzania”, alisambaza taarifa kwa njia ya barua pepe kwa vyombo vyote vya
habari na kumshambulia mwenyekiti wa taasisi ya uwekezaji TPSF kwa kumwita
fisadi, mbinafsi na mfitini wa maendeleo.
Mheshimiwa
Spika, kumekuwepo na hisia kuwa mjadala wa haja ya wazawa kumiliki na kuendesha
sekta ya gesi nchini iliyosimamiwa na taasisi ya uwekezaji nchini TPSF ina
lengo la kutaka kuionesha jamii kuwa serikali kupitia wizara ya Nishati na
Madini na watendaji wengine wa wizara hiyo hawajali masilahi ya wazawa na
hawana utaifa wala uzalendo.
Katika
kuonesha kutokuwa tayari kwa serikali katika kuwasaidia watanzania kumiliki
rasilimali za taisa hili, serikali kupitia waziri mwenye dhamana Profesa
Muhongo alisikika akiwaambia watanzania kupitia kongamano lilifanyika katika
ukumbi wa Nkurumah, chuo kikuu cha Dar es salaam kuwa “Watanzania:
Kampuni za Mengi zimeshikilia vitalu 59 vya madini vyenye ukubwa wa mita za
mraba 3,752.37 (sq km) sawa na Dar es salaam tatu,amevishikilia, ameshindwa
kuviendeleza. Watanzania wanakosa mapato na ajira! Sasa anataka vitalu vya gesi
na mafuta. Je, huu ndio uzawa… tutatoa orodha ya vitalu vya madini vilivyoko
mikononi mwa Mengi ambavyo anafanya ulanguzi. Ukweli utaonyesha ubabaishaji na
ulanguzi wa Mengi wa genge lake.”
Mheshimiwa
Spika, kauli ya serikali
ilitolewa na waziri mwenye dhamana ya Nishati na Madini, inasikitisha jinsi
ambavyo serikali hii ya CCM ina watendaji ambao hawawezi hata kufanya jambo
dogo la utofauti, hoja ya TPSF ni tofauti na hoja ya bwana Mengi kama mtu
binafsi, tamko la TPSF, lilitokana na kikao cha bodi ya taasisi hiyo cha Agosti
28, maoni yaliyo wasilishwa kuhusiana na gesi asilia yalikuwa ya TPSF kama
wadau wakubwa wa uwekezaji. Aidha Katika maoni hayo, TPSF ilisisitiza umuhimu
wa ushirikishwaji wa Watanzania katika uchumi wa gesi na kushauri kusitishwa
ugawaji wa vitalu vya gesi hadi hapo sera ya gesi itakapokuwa tayari.
Mheshimiwa
Spika, serikali hii tayari
katika jambo hili la uwekezaji wa gesi imeonesha msimamo wake, awali serikali
ilisema kinaga ubaga kwamba sheria iliyopo haikidhi mahitaji ya sekta ya gesi
asilia ndiyo maana serikali ikaamua kusimamisha ugawaji wa vitalu vya gesi na
kuamrisha mikataba ipitiwe upya na sera ipatikane. Waziri wa Nishati Septemba
2012 alikaririwa akisema: “Baadhi ya mikataba ni ya ovyo, na inahitaji
kuvunjwa.”Na “Sitovumilia mikataba ambayo haina masilahi kwa nchi na
inawanufaisha wachache.”
Mheshimiwa
Spika, msimamo huo wa serikali
ulianza kwa kuamrisha Bodi mpya ya TPDC kusitisha ugawaji wa vitalu vya gesi
ambao ulipangwa kufanyika Septemba 2012 na kupitia upya mikataba yote. Aidha
miezi michache baadaye, Februari 26, 2013, serikali ilirudia azma yake hiyo
mjini London katika ukumbi wa Chatham kwenye mkutano uliopewa jina la
“Tanzania: An Emerging Energy Producer”.
Katika
hali ya kustajabisha, serikali ilibadilisha mawazo ghafla, na sasa serikali
ilitaka vitalu vigawiwe kabla ya kuwapo kwa sera ya gesi. Waziri wa Nishati na
madini, Prof. Muhongo alinukuliwa na gazeti la Daily News la Agosti 31, 2013
akieleza sababu zake za kutaka vitalu vigawanywe kabla ya kupitishwa kwa sera
ya gesi kuwa ni pamoja na mosi, ushindani wa soko na majirani zetu, akitolea
mfano wa Msumbiji. Pili, sheria ya mwaka 1960 iliyoanzisha TPDC na Sheria ya
Petroli ya mwaka 1980, kwamba zinatosha kusimamia ugawaji wa vitalu,
akimaanisha sera na sheria mpya zitafuata baada ya ugawaji wa vitalu; na tatu,
Watanzania hawana uwezo wa kuwekeza katika sekta hii akimaanisha waachiwe
wageni peke yao.”
Aidha
serikali katika kusisitiza nia hiyo ilisema wafanyabiashara wa Tanzania
wanaweza tu kushiriki biashara ya juisi na soda na hawana uwezo wa kushiriki
katika biashara ya gesi ambayo ni moja ya utajiri unatokana na ardhi ya nchi
yao Tanzania.
Mheshimiwa
Spika, Kambi Rasmi ya Upinzani
Bungeni, inaungana na maoni yaliyotolewa na taasisi ya uwekezaji Tanzania TPSF
juu ya uwekezaji kwenye sekta ya gesi asilia, pamoja na hayo, tunaitaka
serikali kufanya mambo yafuatayo; mosi kutoa hadharani taarifa ya kupitiwa kwa
mikataba yate ya vitalu iliyoagizwa kufanywa na TPDC.
Pili,
kambi rasmi ya upinzani inaitaka serikali kuacha dharau kwa Watanzania kuwa ni
masikini na hawana uwezo huku jukumu la kuondoa huo umasikini likiwa mikononi
mwao, ni kweli kuwa ghara za uwekezaji zinaweza kuwa ni kubwa lakini, kama
tunashuhudia makampuni ya kigeni kama IPTL yakija kuwekeza Tanzania bila mitaji
na yanapewa mikataba, makampuni ya uchukuzi kwenye reli na makampuni lukuki
yakija hapa bila mtaji na kudhaminiwa na serikali, serikali hii inashindwa nini
kuwadhamini Watanzania kuwekeza katika sekta ya gesi asilia?
[…]
Mheshimiwa
Spika, kampuni ya Pan African
Energy Tanzania (PAT) Ilikosa sifa za uaminifu ambapo Kamati ilishauri Mkataba
wa Pan African Energy Tanzania (PAT) usitishwe. Aidha, utekelezaji wa kuvunja
mkataba huu ulipaswa kwenda sambamba na kuhakikisha kuwa taratibu za kisheria
na za kimkataba zinazingatiwa, uwepo wa usalama wa visima na mitambo na uwepo
wa uhakika wa huduma ya upatikanaji wa gesi nchini. Hili lilikuwa ni pendekezo
namba 4 la kamati iliyochunguza uendeshwaji wa sekta ndogo ya gesi asilia hapa
nchini na baadae kuwa azimio la Bunge.
[…]
Mheshimiwa
Spika, Waziri wa Nishati wa
Madini alipokuwa anazindua Bodi mpya ya Shirika la Maendeleo ya Petrol alitoa
maagizo ya kupitia mikataba yote ya utafutaji na uzalishaji wa mafuta kupitiwa
upya baada ya kuonekana ya kuwa ilikuwa na hisia za rushwa na haina maslahi kwa
nchi.
Mheshimiwa
Spika, Aidha maelezo kuwa Muundo
ulishirikisha wafanyakazi wote management, TUICO na Bodi, Kambi Rasmi ya
Upinzani Bungeni Inasema kuwa huo sio ukweli kwasababu muundo uliotengenezwa
ambao ulishirikisha hao hapo juu ulipelekwa Wizara ya Nishati na hadi leo
haujawahi kujibiwa. Muundo unotelekelezwa sasa ni muundo uliotengenezwa na
Wizara na Bodi kwa siri. Kuna vitengo vimefutwa, na kuna kazi zilizofutwa na
wanaozishikilia hawajaelezwa hatima yao.
Mheshimiwa
Spika, Kambi Rasmi ya Upinzani
Bungeni inapenda kupata majibu katika masuala yafuatayo kutoka kwa Waziri wa
Nishati na Madini;
(i)
Ni hatua gani zimechukuliwa kwa waliobainika kuwa walihusika katika kuingia
mikataba mibovu?
(ii)
Mikataba yote ya PSA na hususan ile ambayo inakaribia uzalishaji imeongezewa
“Addendum” za kifisadi zenye vipengele ambavyo havina masilahi kwa nchi ila
vinamnufaisha zaidi mwekezaji? Mikataba iliyoongezewa “addendum” ni ya STATOIL
ambao wapom pamoja nja EXONMOBIL na ile ya BG wakiwa pamoja na OPHIR. Kwa sasa
OPHIL wameuza baadhi ya hisa kwa Kampuni moja kutoka Singapore. Tunaomba Rais
wetu aingilie kati kwani Wizara imethbitisha kutokuwa na uwezo wa kurekebisha
hali iliyopo. Serikali ilishakiri ya kuwa mikataba upande wa madini haikuwa kwa
maslahi ya nchi. Tunaomba Serikali iangalie kwa upana hii mikataba ya utafutaji
na uchimbaji wa gesi kwani kuna kila dalili ya kwamba nchi haitaweza epuka
laana ya gesi kutokana na
mikataba
iliyopo.
(iii)
Badala ya bodi kutekeleza majukumu iliyopewa, kazi yake ni kusafiri nje ya nchi
kila kukicha. Mwenyekiti wake amefanya safari sita nje ya nchi kuanzia Januari
mpaka May 2014 tu. Inatisha.
Mheshimiwa
Spika, kuhusu Utoaji Wa Vitalu Bila Kufuata Taratibu, Shirika la Maendeleo ya
Petroli Tanzania lilitoa vitalu kwa Kampuni ya OPHIR bila kutangaza Tenda,
tunaomba maafisa wote walioshiriki kutoa vitalu kwa Kampuni ya OPHIR
wachukuliwe hatua zinazostahili.
Mheshimiwa
Spika, aliyekuwa Mkurugenzi wa Utafutaji na Uzalishaji wa mafuta na gesi
amejiunga na kampuni ya Ophir. Kampuni hii ilipewa kitalu bila kufuata sheria
za manunuzi, leo mkurugenzi huyu amestaafu amejiunga nayo na kupewa wadhifa
mkubwa. Nchi yetu kweli tutafika!
Mheshimiwa
Spika, Alieshindwa Kuendeleza Kitalu cha Gesi Analindwa. Kampuni ya HYDROTANZ
inayomilikiwa na Bwana SING (SINGASINGA) ambae ndiye aliyenunua IPTL kupitia
kampuni ya PAP ndiye mmiliki wa kampuni ya HYDROTANZ ameshindwa kuendeleza
kitatu alichokuwa amepewa kwa mujibu wa Mkataba. Alistahili kunyang‟anywa
kitalu husika kutokana na kushindwa kukiendeleza ila kutokana na kulindwa na
wizara bado ameendelea kumiliki kitalu husika.
Mheshimiwa
Spika, Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni inajua kuwa kuhusu Viongozi Walioshiriki
Katika Mikataba Mibovu Kama Wa Songo Songo. Cha kushangaza ni kwamba Katibu
Mkuu aliyekuwepo wakati wa utiaji saini mikataba inayosemekana ni mibovu ya
Songo Songo na PAN AFRIKA Mhe. Rutabanzibwa ndiye kwa sasa ni Mwenyekiti wa
Kampuni ya Pan Afrika Tanzania.
Hivi
sasa anafanya mbinu waziwazi za kuisafisha Kampuni hiyo ambayo imeonekana kuwa
na dosari lukuki za kiutendaji na kimaadili. Kampuni ya PAN AFRIKAN ENERGY
inafanya jitihada za makusudi “ku-sabotage” mradi wa bomba la gesi asilia
unaoendelea kwa kutotekeleza majukumu yao mya kuongeza kiwango cha gesi asilia
kinachoweza kuzalishwa kwa ajili ya mradi huu mkubwa wa serikali.
[…]
– JOHN MNYIKA
– UKURASA WA 83- 128 WA HANSARD YA MAJADILIANO YA BUNGE YA 30 MEI 2014
Paul Ngana:
Wadau,
Below is a very good piece written by Zitto sometime ago. In my opinion,
anasahau kitu kimoja, kwenye utafutaji wa oil na gesi kuna kupata na kukosa. Na
ni mara nyingi hawa watu huwa wanakosa, though the success rate is somehow
higher now with advances in technology. Sasa wakipata, some of exploration
costs, can be recovered, depending on agreed PSA. Ikibuma, its your loss. As an
example Shell
to write-off $200 million on Tanzania Well. Now that’s just one well.
Drilling ships for offshore wells can cost up 1 million USD per day. So
depending on the size of your bock, you might have to continue drilling to gain
more data. So yo do the math.
So you can understand why that could be too expensive for individuals. So Prof
Muhongo yuko sawa, vitalu vipo wazi for all to bid. Kama, Mengi na wenzake
wanaweza, kutafuta mitaji kwenye masoko ya hisa (kama alivyoelezea Zitto hapo
chini), please go ahead. Ila wasiseme, kwa sababu nina passport ya Tanzania,
nipewe upendeleo. Mimi hicho sikubaliani nacho. Ndio wazawa wapewe kipaumbele,
ndio maana kuna local content policy, ila tusijiumize kisa uzalendo. Tuangalie
mwisho wa siku taifa tunapata nini. Hela zinazopatikana ziwekwe kwenye
sovereign wealth fund kama wenzetu “Sovereign wealth
Fund”, halafu matumizi yaamuliwe bungeni.
Pia Muhongo yuko sawa, kwamba TPDC awe mwakilishi wa watanzania, there are many
successful examples like Saudi Aramco (Saudi Arabia), Petronas (Malaysia),
Petrobras(Brazil), PVDSA (Venezuela), Gazprom(Russia) you name it. Ni kweli
ndio kuna baadhi ya nchi ambazo unasikia watu binafsi wana hivi vitalu. Kwa
mfano kule Nigeria na Russia, utaona hao watu binafsi ni marafiki wa watu
jeshini au high level ranking politicians. And some of them, wanakaa na hivi
vitalu, halafu wanaziuza tena. Others wanataka quick wins, wanaenda nje
wanachukua contractors, na hiyo hela inaishia mifukoni kwao na hakuna faida kwa
taifa. Kwa hiyo hapo [juu] Muhongo yuko sawa in my opinion.
Pia alichosema Zitto kwenye conclusion yake ni muhimu sana, uchafuzi wa
mazingira ukitokea Mtwara, watakaoumia ni hao watu wa mtwara na sio watu wa
arusha. Na kwa uzoefu wangu mdogo kwenye hii sekta, utaona kuwa kwenye maeneo
yenye uchimbaji wa gesi/oil huwa wanakuwa masikini kuliko maeneo mengine ya
nchi hizo. Wanaofaidika na hizo hela huwa wanaku mbali kabisa na hayo
maeneo.
Kitu kingine, skyrocketing of costs of livings, pia kuna issue ya uharamia,
target areas for terrorist attacks, majangili etc. Yaani, majanga juu ya
majanga. Nawaonea sana huruma hao watu wa Mtwara, Lindi. Imekula kwao.
Paul
————-
by Zitto Kabwe
Nani anamiliki rasilimali za nchi
NANI ana miliki ya dhahabu yote iliyogunduliwa Tanzania hivi sasa? Nani ana
miliki yote ya misitu iliyopo nchini? Nani ana miliki ya gesi asilia
iliyogunduliwa hivi karibuni mikoa ya Pwani, Lindi na Mtwara? Watanzania
wachache sana wanayo majawabu ya maswali haya.
Inasikitisha hata Watanzania tuliopewa fursa ya kuwaongoza wenzetu milioni 45
hatuna majawabu na wala hatutafuti majawabu ya swali hili. Viongozi tunawaambia
wananchi kwamba “maliasili ya nchi ni mali ya umma.” Ni kweli mali ya umma?
Umma ni nani? Hebu tuangalie mfumo wetu wa miliki ya rasilimali za madini,
mafuta na gesi asilia. Katiba ya sasa ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania haisemi lolote kuhusu
‘miliki’ ya utajiri wa taifa. Isipokuwa katika ya kifungu cha tisa (c) na (i)
na ibara ya 27 (1) suala la maliasili ya nchi limewekewa masharti ya Katiba.
Ibara ya 9 (c) inasema shughuli za serikali zitatekelezwa kwa njia ambazo
zitahakikisha utajiri wa taifa unaendelezwa, unahifadhiwa na unatumiwa kwa
manufaa ya wananchi wote kwa ujumla na pia kuzuia mtu kumnyonya mtu mwingine.
Ibara ya 9(i) inasema matumizi ya utajiri wa taifa yatatilia mkazo maendeleo ya
wananchi na hasa zaidi yanaelekezwa kwenye jitihada ya kuondosha umasikini,
ujinga na maradhi.
Ibara ya 27 inahusu wajibu wa raia kulinda maliasili ya Jamhuri ya Muungano.
Ibara ya 9 kuna masharti ya Katiba ya kujenga Ujamaa. Hakuna ibara ya Katiba
inayozungumzia ‘miliki’ ya utajiri wa taifa. Suala hili liliachiwa sheria
zilizotungwa na Bunge. Kwa suala utajiri tuliochagua kufanyia kazi katika
makala haya sheria hizo ni Sheria ya Madini ya Mwaka 2010 na Sheria ya
Utafutaji wa Mafuta ya Mwaka 1980.
Nani anamiliki madini nchini?
Sheria ya madini ya mwaka 2010 imesema madini ni mali ya umma, hata hivyo,
imeweka masharti ya kuhamisha umiliki huu kwa watu na kampuni binafsi kwa
mtindo wa leseni. Dhahabu ni mali ya umma pale tu utafutaji wake na hatimaye uchimbaji
haujatolewa kwa mtu binafsi. Leseni ikishatolewa miliki (mineral right)
inahamia kwa mwenye leseni na hapo taifa linabakia kupata mrabaha tu kama tozo
ya uvunaji wa rasilimali hii.
Kiuhalisia, mfumo huu unaruhusu maliasili ya nchi kumilikiwa na watu binafsi
wawe raia wa Tanzania au la. Angalia mfano huu.Kampuni iitwayo ZiMinerals LTD
kutoka Canada inakuja Dar es Salaam katika Wizara ya Nishati na Madini na
kuomba leseni ya kutafuta dhahabu huko Kahama. Wizara inampa leseni ya
utafutaji ya mamia ya kilometa za mraba. ZiMinerals inakwenda kujiandikisha
katika soko la mitaji la huko Australia na kuanza kukusanya fedha kwa kutumia
leseni ya utafutaji dhahabu Tanzania.
Ikishapata fedha inaanza kazi ya kutafuta na baada ya kupata kiwango cha dhahabu
wanatangaza na bei ya hisa za kampuni hii zinapanda maradufu. Serikali inaipa
kampuni hii leseni ya kuanza kuchimba na kampuni sasa inaanza kuuza dhahabu
duniani au inauza miliki hii kwa kampuni nyingine kubwa na yenye uzoefu zaidi
au mtaji zaidi. Kitendo cha ZiMinerals kuuza hisa zake huko Australia tayari miliki ya
rasilimali iliyopo Tanzania inakuwa inamilikiwa na wananchi wa nchi hiyo au
raia wa nchi nyingine yoyote duniani mwenye kuweza kununua hisa katika soko
ambalo hisa za ZiMinerals zinauzwa.
Hivi ndivyo inafanyika. Wanakuja watu hawana hata nguo ya kubadili, wanapata
leseni wanakwenda kwao kukopata fedha kwenye masoko ya mitaji na wanakuwa
matajiri wakubwa kwa kutumia miliki ya rasilimali za Tanzania na Watanzania
wanabaki fukara.
Hivyo ndivyo ilivyofanyika Bulyanhulu, Kampuni ya Sutton Resources ilipewa
leseni, ikaenda sokoni kufanyia biashara leseni hiyo, wakawekeza dola za
Marekani 20,000 kwenye utafutaji kisha wakauza leseni yao kwa Kampuni ya
Barrick Gold, kwa Dola milioni 348. Kwa hiyo tunaposema maliasili hii ni ya
taifa tunajidanganya tu. Ukishatoa leseni kinachobaki cha taifa ni ule mrabaha
wa asilimia nne tu kwa mujibu wa sheria mpya ya madini ya mwaka 2010
iliyoshinikizwa na sakata la Buzwagi.
Kwa upande wa rasilimali ya gesi asilia na mafuta hali ni tofauti. Miliki ya
umma inakuwa ni milki ya serikali na inasimamiwa na Shirika la Umma la Mafuta,
hivi sasa TPDC. Kwa hiyo, kwa mfano, kampuni ya ZiGas Limited kutoka Australia
inapokuja hapa nchini na kuruhusiwa kutafuta mafuta au gesi na kisha kuchimba,
inakua imeajiriwa na TPDC.
Ikienda kule Australia kutafuta fedha itauza kwenye soko ile asilimia yake tu,
mara nyingi ni asilimia kati ya 80 na 85. Lakini pia hata ikiuza mafuta au
gesi, kulingana na kiwango cha mauzo hayo, asilimia sio chini ya 60 ya mauzo
baada ya kuondoa gharama za uzalishaji inachukuliwa na TPDC (serikali).Hata
hivyo tofauti na madini, mrabaha sasa unalipwa na TPDC kwa serikali na sio hii
kampuni ambayo ni kama mkandarasi (contractor) wetu. Kwenye gesi tunaweza kusema
mali yetu, ingawa si kwa asilimia 100.
Kwa nini mifumo tofauti?
Hakuna maana yoyote ile zaidi ya umazwazwa (ujuha) tu. Kwa nini kampuni za
ndani ama za serikali au za watu binafsi haziendi kutafuta fedha kwenye masoko
ya mitaji na kufanya utafutaji na kisha kuvuna utajiri huu? Ni ujuha tu maana
yote yanawezekana.
Walipokuja Ophir Energy hapa Tanzania na kupata mkataba wa kutafuta mafuta
kwenye kitalu namba moja kule Bahari ya kina kirefu mkoani Mtwara, walikwenda
kuuza hisa kwenye soko la mitaji na hisa moja ilikuwa inauzwa senti nne ya
Pauni ya Uingereza (4 pences). Huu ulikuwa ni mwaka 2006. Mwaka 2011 baada ya kupata gesi asilia kwenye visima kadhaa, hisa moja ya
kampuni hii ilifika senti 654 ya Pauni (654 pences). Licha ya bei kupanda namna
hii lakini pia waliuza sehemu ya kampuni yao kwa Kampuni ya BritishGas na
kupata mabilioni ya pauni za Uingereza bila Tanzania kupata lolote licha ya
biashara hii kuwa ni mali iliyopo Tanzania.
Hivi kweli baadhi yetu tunasimama na kusema gesi asilia mali ya umma? Dhahabu
mali ya umma? Almasi mali ya umma?
Tunawadanganya wananchi. Lazima kufanya mapinduzi ya kifikra na kivitendo.
Maandamano ya watu wa Mtwara yasukume . Watanzania kufukua zaidi kuhusu
unyonyaji wa utajiri wa nchi. Mapinduzi ni lazima.
Katiba ya nchi sasa iseme kinagaubaga kuwa rasilimali ni mali ya wananchi (sio
mali ya umma). Miliki (mineral right) ya utajiri wa nchi iwekwe kwenye mikono
ya wananchi wenyewe kwenye maeneo ambayo rasilimali imepatikana au inatafutwa.
Serikali itakuwa ni msimamizi wa uvunaji wa rasilimali hii kwa manufaa ya
wananchi wote. Wananchi wa eneo ambalo rasilimali inatafutwa au imepatikana wawe na haki ya
kuridhia kuvunwa kwa rasilimali hiyo kabla Serikali Kuu haijatoa ruhusa ya
kuvunwa kwa rasilimali hiyo (The right of prior informed consent).
Mapinduzi haya ya umiliki wa rasilimali za nchi kutoka kwa serikali kwenda kwa
wananchi wa maeneo yenye rasilimali kutawezesha mrabaha wote unaolipwa na
kampuni za uvunaji wa rasilimali kulipwa kwa wananchi hawa kupitia serikali zao
za mitaa na majimbo (provinces).
Mapato haya ndio yatafidia kuondolewa kwa wananchi kwenye mashamba yao kupisha
uvunaji huu au kufidia samaki wanaopotea kutokana na uchimbaji mafuta na gesi
kwenye bahari. Ieleweke kwamba mrabaha si kodi bali ni tozo la fidia kwa
kunyonya (kuvuna) mali katika eneo husika.
Viongozi tunaposema maliasili ni mali ya taifa tuna maana fedha zitokanazo
na maliasili ni mali za taifa. Hivi tumewahi kujiuliza madhara ya uharibifu wa
mazingira nayo ni madhara kwa taifa zima?
Kwa mfano madhara ya kuchimba mafuta kule Mtwara, madhara ya kimazingira
ikiwamo sumu yanamilikiwa kwa pamoja kati ya Kigoma na Mtwara au Kigoma
itafaidi tu dola zitakazotokana na gesi ya Mtwara lakini Mtwara itaumia peke
yake na uharibu mkubwa wa mazingira unaotokana na uchimbaji wa gesi.
Tusiwe na midomo mikubwa kuona fedha za kugawana nchi nzima na kufumbia macho
uharibifu mkubwa wa mazingira na upoteaji wa maisha unaowaathiri Watanzania
wanaoishi kwenye maeneo fedha hizo zinatoka.
Sumu katika Mto Tigite kule Tarime haigawanywi kwa Watanzania wote isipokuwa
mapato ya dhahabu, japo nayo ni kidogo tu maana miliki ni ya kampuni binafsi,
inayovunwa na kuchafua maji ya mto huu inagawanywa kwa Watanzania wote. Hatuwezi kuendelea kuwa na taifa ambalo Wilaya ya Geita yenye mgodi mkubwa
zaidi wa dhahabu barani Afrika, ukiondoa Ghana na Afrika Kusini lakini ni
masikini zaidi Tanzania. Halafu tunasema maliasili ni mali ya taifa. Turudishe
rasilimali kwa wananchi.
Sabatho Nyamsenda:
Mie sioni kwa nini debate ya Mengi na Muhongo itulazimishe kuchukua upande ama
wa Mengi au wa Muhongo. Mie sifungamani na yeyote, japo napigia chapuo dola
kuwa na uhodhi katika uwekezaji wa uchumi.
Tarehe
9 Desemba 2013 kulikuwa na Kongamano la Udasa kuadhimisha kumbukizi ya siku ya
uhuru wa Tanzania Bara. Kongamano lile liliwaleta pamoja Mengi na Muhongo.
Mwenyekiti wa Udasa wakati huo (ambaye baadaye alijiteua kuiwakilisha
Udasa katika Bunge la Katiba) anafahamika kama kada wa CCM, na katibu wake ni
sympathiser wa upinzani. Katika mjadala ule Muhongo alipewa nafasi ya mwisho
kuzungumza na akapangua hoja zote za Mengi na kisha kulipua bomu kuwa Mengi
anamiliki ardhi ambayo ni mara tatu ya mkoa wa Dar es Salaam.
Baada
ya bomu la Muhongo washiriki waligawanyika katika makundi mawili. Vijana wa CCM
wakiwa nyuma ya Muhongo, na wale wa CDM/CUF wakiwa nyuma ya Mengi. Likaitishwa
Kongamano la pili (kwa kuwa la kwanza lilikuwa limekwisha) hapo hapo Nkrumah,
huku viongozi wa upinzani (Lissu, Mnyika, Esther Wassira na Mtatiro) wakipanda
jukwaani na Mengi, na kusema kuwa Muhongo ni mwongo. Muhongo kabla hata
Kongamano la pili halijaanza, Muhongo akakata umeme wake, huku askari wakitumwa
kuwaondoa washiriki ukumbini.
Nje
ya ukumbi vijana wa vyama walitaka kupigana. Niliingilia ugomvi wa kundi moja
na kuwauliza, “Hivi mnachopigania ni nini hasa?” Hawakuwa na hoja. Baada ya
kutoa mhadhara mfupi, nikahitimisha: “Muhongo ni mwongo, na Mengi kaficha
mengi”! Nikawaambia kama wanapigania maslahi ya wanyonge basi wasichukue
hizo pande mbili.
Na
kwa kweli, ni pande mbili zenye lengo moja. Muhongo na Mengi hawatofautiani:
wote wanapigia chapuo uwekezaji toka ughaibuni. Wanapotofautiana ni nani awe
dalali? Mengi anasema nafasi ya udalali ya TPDC ichukuliwe na “wazawa”. Muhongo
anasema ifanywe na dola kupitia TPDC. Kwa hiyo hapo bado kuna dhana ya uchumi
tegemezi, ambao mashabiki wake (akina Mwapachu) wanasema “pesa tutapata toka
huko nje”.
Zitto Kabwe:
Ni
kwa vipi Muhongo anataka TPDC iwe ndio dalali wa dola?
Mjadala
mzima huu upo katika msingi wenye nyufa kwani suala sio Mengi v Muhongo. Suala
ni ‘nani mmiliki wa rasilimali hizi za asili?
TPDC
ni mtoa leseni na msimamizi tu wa vitalu. TPDC imepewa haki ya kumiliki mpaka
20% ya hisa za kampuni za uwekezaji katika sekta (kwa kununua hisa hizo). Pia
TPDC ni mpokeaji wa fedha za Serikali zinazotokana na ‘profit oil/gas ‘ pamoja
na mirahaba. ‘ hadithi ‘ ni pale ambapo Watanzania wanaambiwa kuwa TPDC
inamiliki kwa niaba yetu, kivipi? Wapi?
Wakati
wa zabuni ya kugawa vitalu vipya Rais alinukuliwa akisema kuwa ‘ TPDC itakuwa
na hisa 80% kwa niaba ya watanzania ‘ kitu ambacho kilionyesha ujuzi mdogo sana
wa viongozi wetu kwenye suala la mafuta na gesi. Zipo wapi hizo hisa 80%? Hii
hadithi inayorudiwa rudiwa bungeni na kukaririwa bila kuhojiwa. Hakuna kitu
kama TPDC kumiliki kwa niaba yetu. TPDC ni mpokeaji wa mgawo wa mrahaba na
mafuta au gesi Asilia ya ziada. Umiliki wa mpaka 20% ni ‘ option’ iwapo
TPDC itataka kununua. Option hii ipo kwenye mikataba yote, apewe mtanzania
kitalu au mgeni. Lakini ni option ambayo sio ya ‘ lazima ‘ na sio ya bure.
Ni
dhahiri Watanzania wanapaswa kumiliki makampuni haya. TPDC inapaswa kuwa na
kampuni tanzu ( Niliwahi kushauri mwaka 2010 kampuni hii kuitwa PetroTan).
Kampuni hii tanzu ikamiliki hizo haki za TPDC katika kampuni za utafutaji na
50% ya kampuni hii ikauzwa kupitia soko la hisa na nusu iliyobakia ikamilikiwa
na TPDC au Msajili wa Hazina.
Hadithi ni kuwaambia watanzania kuwa wanamiliki kupitia TPDC wakati sio kweli.
Ni hoja ya kupinga hoja lakini iliyojengwa kwenye msingi dhaifu kwa pande zote
zenye kushindana hoja hizo
George Fumbuka:
Kwa
uelewa wangu TPDC ni DEPOSITORY ya share za Watanzania, kama UTT walivyopewa
hisa za TBL na TCC kama seed capital. Baadaye TPDC watadwnloand hisa hizo kwa
wananchi. Katika hiyo 80% ndiyo ya kudownload. Where is the problem?
Demere Kitunga:
Hiyo
80% inatoka wapi kama wanaruhusiwa 20% tu, labda kama sikumuelewa vizuri Zitto.
Zitto Kabwe:
Huo
uelewa wako unatokana na nini? Hizo ni hisia zako au unataka iwe hivyo lakini
sio uhalisia.
Hakuna
sheria inayosema TPDC ni depository
Salim Khatri:
Zitto, Twende taratibu. Mimi nikiwekeza hela yangu kwenye kampuni
nachotaka zaidi humo ni hiyo faida inayotokana na hiyo kampuni. Na nikisia kuwa
hiyo kampuni ina tabia ya kuingiza hasara badala ya faida, mimi hiyo kampuni
sitawekeza. Naamini hata wewe hautawekeza kwenye hiyo kampuni. Hivyo hivyo kama
Taifa (siyo individual wenye kuyatolea macho hayo mafuta na gesi) tunachojali
na kutaka ni kuwa hiyo faida wanayopata hayo makampuni pale wanapochimba hayo
mafuta na gesi na sisi tunafaidi, again tunafaidi kama Taifa na siyo individuals,
yaani faida hizo ziingie kwenye mfuko wa serikali zikajenge hospitali, shule na
mambo mengine ya maendeleo. Kumiliki kampuni (“all affairs” kama zile za IPTL)
ni pamoja na kumiliki madeni na matatizo ya kampuni hiyo. Nani anataka hayo?
Kumiliki asilimia kadhaa ya faida ni bora kuliko kumiliki hisa za
kampuni. Huo ndiyo umilikaji anaozungumzia Rais Jakaya Kikwete. Kwa model PSA
Tanzania kama nchi itakuwa inamiliki faida ya mpaka 80% yanatokana na shughuli
za kuchimba mafuta/gesi. Mafuta yetu, wanachimba wao. Faida tunagawana kwa
mujibu wa uzalishaji. Kuna ubaya gani hapo?
[…]
Kwanini tuitake serikali iwekeze hela zetu ama ikakope kuweka maisha
yetu rehani kwenye biashara ambayo ni “kamari” tu? Alex Kobalyenda kauliza
swali la kimsingi kabisa “If we can’t feed ourselves, who will agree tukope to
gamble?”
Nafikiri wengi wengu hampendi huu mjadala uwe kati ya yale anayoyasema
Prof. Muhongo na yale yanayodaiwa na Mengi kwa sababu hizo ndizo hoja kuu
mbili. Mmoja anataka Tanzania kama taifa lifaidike collectively, mmoja anataka
few selected Tanzanians wafaidike zaidi. Na ndiyo hoja za eti wanaounga mkono
hoja ya Prof. Muhongo “wana wivu”.
Dr. Antipas Massawe:
Watanzania
wanao uwezo mkubwa sana wa kuwekeza kwenye sekta ya utafutaji na uchimbaji wa
mafuta ya petroli na gesi asilia hapa nchini kwa sababu mtaji unaohitajika ni
sehemu kidogo mno ya thamani ya hatimiliki za vitalu husika kwenye utafutaji na
uchimbaji wa hiyo raslimali yetu ya madini. Kuwapa watanzania hatimiliki
za vitalu hivyo ni kuwapa uwezo wa kuwagawia wawekezaji wa kigeni sehemu kidogo
tu ya hisa kwenye hatimiliki hizo ili wawekeze mtaji kidogo unaohitajika
kuvijengea vitalu husika uvutio kwa wawekezaji wengine matajiri zaidi na/au
taasisisi zinazotoa mikopo wa kuwekeza mtaji husika kwenye kukamilisha
utafutaji na kuanzisha uchimbaji wa vitalu vitakavyogundulika kuwa na raslimali
zinazochimbika kwa faida.
Kilichotakiwa
kifanyike ni serikali kuwezesha ubia kati ya watanzania na serikali yao
(kupitia TPDC) kwa kuupa hatimiliki za vitalu vyote vya mafuta ya petroli na
gesi asilia uweze kugawa sehemu kidogo tu ya hisa kwenye hati miliki hizo kwa
wawekezaji wa kigeni watakaochangia mitaji midogo inayohitajika kuvifanya viwe
kivutio kwa wawekezaji wengine wakubwa na/au taasisi zinazotoa mikopo
kujinunulia sehemu nyingine ya hisa za vitalu hivyo kwa njia ya kuwekeza mtaji
utakaohitajika kukamilisha utafiti na kuanzisha uzalishaji kwenye vitalu
vitakavyogundulika kuwa na rasilimali zinazochimbika kwa faida.
Tunapogawa vitalu vya utafutaji kwa wageni tumewapa pia mtaji wa
kuviendeleza ambao ni sehemu kidogo sana ya dhamani ya hatimiliki ya vitalu
hivyo kwenye soko. Wote wanaosema watanzania hawana uwezo wa kuwekeza
kwenye sekta ya utafutaji na uchimbaji wa mafuta na gesi asilia hapa nchini ni
wasiolewa biashara hiyo inakwendaje, na hivyo kutokuwa na uelewa wa namna gani
serikali ingeweza kuwawezesha watanzania kuwa wamiliki wakuu kwenye biashara
hiyo na kuliletea taifa manufaa makubwa zaidi. Nimechangia mada kadhaa
kuhusu namna watanzania wanavyoweza kushiriki kwenye utafutaji na uchimbaji
madini hapa Tanzania na kuiletea manufaa mkubwa zaidi kwenye blog ya GOXI
hapa: Antipas Massawe’s Blog – GOXI <goxi.org/profiles/blog/list?user=39h14kv44tucu>
Chambi Chachage:
“TPDC will
continue to attract International Oil Companies through promotional
campaigns as a strategy to maintain the momentum of petroleum exploration in
the country….TPDC will continue to participate in Production
Sharing Agreement negotiations with International Oil Companies interested to
take Exploration Licences on basis of available data and information”
– Tanzania Petroleum Development Corporation (TPDC),14
July 1998
“To
encourage investments and attract international oil companies to operate in the
country, Tanzania shall strive to maintain competition in the licensing process
through carefully planned and transparent license bidding rounds and regular
review of fiscal framework. The rounds should aim at attracting a variety of
technically and financially qualified applicants. These principles on
licensing shall be entrenched in legislation…The rapid growth of
the petroleum upstream sub-sector, and huge natural gas discoveries, prompted
the need to review and update the key legislation governing petroleum
upstream in the light of this policy so as to facilitate its implementation,
appropriately capture the recent changes in the industry and prudently manage
the exploration, development and exploitation of petroleum in the
country. The provisions that need to be revisited or added in the
legislation include the following …. Review exploration license
period. ii. Review the exploration licence acreage size. iii. Government
benefits from all transactions of assets related to in-situ petroleum
resources…e) Provision for the clarification of roles and responsibilities of
the various institutional entities involved in the petroleum activities
(Ministry, regulator, national oil company)….” – The
National Petroleum Policy of Tanzania, Draft, 3
July, 2014
“Mheshimiwa
Spika, sheria ambayo tunayoileta na nimeshaongea na wakuu
wangu wote kwamba hii gesi iliyogundulika tusipokuwa waangalifu tunaweza
tusifaidike. Ndiyo maana ni lazima tuwe waangalifu kwa sababu
huyu mtu
akivuna gesi, sasa tuamue je, hizo fedha kama kitalu ni chake ni fedha zake na
familia yake, lakini kama ni za TPDC ni zetu wote, za Watanzania wote. Kwa hiyo
msidanganywe na hadithi yoyote na tutakuja hapa, sheria tunayoileta
hapa ya sovereign fund ni kwamba zile fedha hata Hazina hawatazichukua
zile fedha kwamba yamepatikana mabilioni tunaenda tunayamwaga yote pale Hazina,
hakuna kitu kama hicho. Patatengenezwa mfuko maalum na fedha zile hazitatoka
bila ya uthibitisho wa Bunge”- Minister of Energy &
Minerals, 30 May 2014
“TPDC
ni mtoa leseni na msimamizi tu wa vitalu. TPDC imepewa haki ya kumiliki mpaka
20% ya hisa za kampuni za uwekezaji katika sekta ( kwa kununua hisa hizo ). Pia
TPDC ni mpokeaji wa fedha za Serikali zinazotokana na ‘ profit oil/gas ‘ pamoja
na mirahaba. ‘ hadithi ‘ ni pale ambapo Watanzania wanaambiwa kuwa TPDC
inamiliki kwa niaba yetu, kivipi? Wapi? Wakati wa zabuni ya
kugawa vitalu vipya Rais alinukuliwa akisema kuwa ‘ TPDC itakuwa na hisa 80%
kwa niaba ya watanzania ‘ kitu ambacho kilionyesha ujuzi mdogo sana wa viongozi
wetu kwenye suala la mafuta na gesi. Zipo wapi hizo hisa 80%?
Hii hadithi inayorudiwa rudiwa bungeni na kukaririwa bila kuhojiwa. Hakuna kitu
kama TPDC kumiliki kwa niaba yetu. TPDC ni mpokeaji wa mgawo wa mrahaba na
mafuta au gesi Asilia ya ziada. Umiliki wa mpaka 20% ni ‘ option’ iwapo
TPDC itataka kununua. Option hii ipo kwenye mikataba yote, apewe mtanzania
kitalu au mgeni. Lakini ni option ambayo sio ya ‘ lazima ‘ na sio ya
bure.” – Mwenyekiti wa PAC, 12
January 2015
Zitto Kabwe:
Pia tusichanganye hisa na mgawo wa mapato (profit gas or oil). Mjadala
hapa ni umiliki wa watanzania au ushiriki wa watanzania katika sekta.
[…]
Pia ninadhani mjadala huu ni muhimu sana kwa ajili ya kuona namna
watanzania wanaweza kushiriki katika sekta hii. Napendekeza mjadala uitwe ‘
Watanzania na Sekta ya Mafuta na Gesi’
Salim Khatri:
Kuna faida gani ya kumilika hisa za kampuni (advantage) dhidi ya kupata
mgawo wa mapato (profit) ya hiyo kampuni?
[..]
Dr. Antipas Massawe:
Hapana, kumiliki hisa kadhaa za hatimiliki za vitalu vya mafuta ya petroli na
gesi asilia kuna manufaa makubwa zaidi ya kuwa na hisa ya faida itakayopatikana
kutokana na uvunaji kwenye vitalu vitakavyogundulika kuwa na rasilimali
inayovunika kwa faida.
Kuwa na sehemu ya hisa za hatimiliki za vitalu kunamwezesha mwenye
nazo azitumie kama rehani ya kujipatia mikopo kwa ajili ya kuwekeza kwenye
miradi mingine inayozaa faida kubwa, ya uhakika na kwa haraka zaidi mara kadhaa
na kujipatia faida kubwa maradufu ya thamani ya hisa zake kwenye hatimiliki za
vitalu husika ambazo bado ziko mikononi mwake au thamani ya rasilimali yote
iliyomo kwenye vitalu husika.
Kuwa na sehemu ya hisa kadhaa za hatimiliki za vitalu hivyo pia
humwezesha kuzitumia kama reheni ya kujichukulia mikopo kwa ajili ya kuwekeza
kwenye biashara nyingine zenye kuleta faida kubwa na kwa haraka zaidi hata kama
vitalu husika vitakuja vionekane havina rasilimali yoyote inayovunika kwa faida.
Kwa hiyo faida kubwa na yenye maana kubwa zaidi kwenye sekta ya mafuta
na gesi ni ile inayotokana na utumiaji wa hisa kwenye hatimiliki za vitalu
husika kama rehani ya kujichukulia mikopo kwa ajili ya kuwekeza kwenye miradi
mingine yenye faida kubwa, ya haraka na ya uhakika zaidi mara kadhaa huku hisa
za mhusika kwenye hatimiliki ya vitalu husika kwenye utafutaji unaoendelea
zikiendelea kubakia palepale.
Ndio maana wawekezaji wakishagundua gesi huwa wakiwauzia wawekezaji
wengine watakaochimba ili kwenda kuwekeza kwenye kujipatia hisa nyingine nyingi
zaidi kwenye vitalu vingine vingi zaidi vya utafutaji ili waweze kuendelea
kutumia hisa hizo kama rehani ya kujichukulia mikopo kwa ajili ya kuwekeza
kwenye miradi mingine yenye kuleta faida kubwa, ya haraka na ya uhakika zaidi
huku wakisubiria kuuza hiza zao na kujipatia faida kubwa kwenye vitalu
vitakavyokuja kugundulika vinachimbika kwa faida.
Bonanza kwenye biashara ya madini (hasa mafuta na gesi) hupatikana kwa
njia ya kutumia hisa kwenye hatimiliki za vitalu husika kwenye utafutaji
unaoendelea kama rehani ya kujichukulia mikopo ya kuwekeza kwenye
miradi mingine inayoleta faida kwa haraka zaidi, na kuuza hisa kwenye hatimiliki za vitalu vitakavyokuja kugundulika kuwa vina rasilimali inayochimbika
kwa faida, na mtaji utakaopatikana ukaendelea kuwekezwa kwa kwenye kujipatia
hisa za hatimiliki kwenye vitalu vipya vya mafuta na gesi na sio kusubiria
mgawo wa faida itokanayo na uchimbaji ambayo huwa ni kidogo sana.
Wachimbaji huwa wakiendelea na biashara yao ya uchimbaji ingawa
hawapati faida kubwa kama wanaocheza na hisa kwenye hatimiliki za vitalu vya
utafutaji kwa sababu tu uchimbaji ndiyo taaluma wanayoijulia vizuri zaidi. Wenye kupata faida kubwa kwenye uchimbaji ni wale wanaochangia mitambo, huduma na vifaa vingine husika kwenye shughuli hiyo ya
uchimbaji.
TUSISAHAU KWAMBA MITAJI HUSIKA KWENYE UTAFUTAJI NA
UCHIMBAJI WA MAFUTA NA GESI NI SEHEMU KIDOGO SANA YA THAMANI YA HATIMILIKI ZA
VITALU HUSIKA.
Kwa hiyo Tanzania inapoteza kwa kiasi cha kutisha pale ilipokwepa
kujibakizia hisa kubwa kwenye hatimiliki za vitalu husika kwenye utafutaji wa
mafuta na petrol unaoendelea na badala yake ikaamua isubirie mgawo wa faida
itakayopatikana na uchimbaji kwenye vitalu vitakavyokuja kugundulika kuwa na
rasIlimali inayochimbika kwa faida ambAvyo ni chini ya 1% ya vitalu vyote husika
kwenye utafutaji wa mafuta na gesi ambavyo vyote huwa vikiwaletea wenye hisa
kwenye hatimiliki zake faida kubwa pale hisa hizo zinapotumika kama rehani kwenye
kujichulia mikopo ya kuwekeza kwenye biashara nyingine zinazoleta faida kubwa,
ya uhakika na haraka zaidi mara kadhaa wakati utafutaji kwenye vitalu ukiwa
bado unaendelea.
Salim Khatri:
Ahsante kwa majibu yako. Naona hapo umeonyesha faida tu ya biashara ya
“exploration” na sana sana faida ya kuweza kupata mkopo kutumia hati miliki za
vitalu kama rehani (ambayo bado nina mashaka kama kuna benki zinatoa mikopo ya
namna hiyo na kuchukulia “kitalu” kama security hasa ukizingatia benki zetu
zinataka “tangible assets” kama security). Kwenye exploration ni kamari ama
“pata potea”, aidha unapata gesi/mafuta ama hupati kitu baada ya kutumia
mabillioni kuchungulia huko chini. Nafikiri hapo ni wazi serikali yetu haiko
tayari kucheza huo upatu/kamari. Prof. Muhongo kasema katafute wawekezaji
ingieni nao ubia mkashindanie hizo. Hakuna anayekatazwa.
Swali langu liko kwenye uchimbaji. Kumiliki hisa za kampuni zina faida
gani za ziada (advantage) juu ya kupatiwa mapato ya “gesi ya faida” (siyo faida
ya kampuni)?
Chambi Chachage:
Kwa hiyo
“mgawo” wa mapato na “umiliki” wa chanzo cha mapato hayo
haviendani? Toleo hilo la rasimu ya sera lililotoka miezi miwili tu baada ya
hayo maneno ya Waziri yenyewe haivihusianishi? Haipaswi kuvihusianisha kama
Waziri alivyovihusianisha? Hadithi yao ni nini
– hayo mabadiliko waliyotaka kuleta 2014 au
hicho kilicho(kuwe)po?
“Mheshimiwa
Spika, gesi asilia na mafuta: Napenda kurudia tena hakuna Mtanzania aliyezuiwa,
hayupo wala hatujamzuia Mtanzania yeye akatafute kampuni
waje naye akiwa na ubia hatujazuia, na tuna kampuni ya Watanzania
ambayo tayari inafanya kazi na Wa-Australia na wote hata wao wenye kampuni
hiyo walikiri kwamba hawana fedha, hawana teknolojia ndiyo maana
wametmafuta kampuni ya Australia wafanye nayo kazi. Kwa
hiyo ndugu zangu kama nia ya mtu ni kitalu, wewe njoo na
wawekezaji mshindane. Lakini nataka kusisitiza tena haitatokea kwamba kuna mtu
atapewa kitalu yeye na familia yake, haiwezekani! Na hii hata mtu aandike
asubuhi na mchana, aimbe, haiwezekani! TPDC ndiye anayetuwakilisha, anawakilisha
Watanzania wote tajiri na maskini, lakini hamna vitalu vya familia hapa… na
ndiyo maana kama tunakuwa na sovereign fund ni hatari sana kuruhusu mtu na
familia yake awe na kitalu. Haya yote ndiyo nilikuwa nataka ayaweke kwenye
bajeti, sasa yakawa ni hadithi tu” – Minister of Energy &
Minerals, 30 May 2014
|
“The |
Zitto Kabwe:
Mgawo wa mapato (production sharing) ni tofauti sana na umiliki wa
kampuni. Tofauti kubwa. Hata kama TPDC isingepewa haki ya kumiliki hisa hizo
mpaka 20% bado mgawo wa mapato ungekuwa vile vile tu.
Sera hizo ni hadithi kubwa zaidi. Sera ya upstream? Au unasemea sera ya
uchuuzi? Sera ngapi za Tanzania ni hadithi tu, zinatungwa na kuwekwa kwenye
makabati.
Sheria ya gesi ipo wapi? Sheria ya utafutaji mafuta (Mpya ) ipo wapi?
Sera ya matumizi ya fedha ipo wapi? Natural gas master plan ipo wapi?
Hadithi njoo uwongo njoo. Porojo tu
—
MJADALA UNAENDELEA KWENYE: