Kuna mchumi anadai tatizo letu Waafrika ni kuwa tumejikita zaidi katika kupewa/kusambaziwa (supply) misaada (aid) kuliko kudai/kutaka (demand) mtaji (capital) hivyo tunaishia kuwekeza (invest) kwenye vitu ambavyo havileti matokeo (returns) makubwa au faida (profit) nyingi. Anaendelea kusisitiza kuwa kudai/kutaka/kutafuta kwetu mitaji (capital) ni kwa kiwango cha chini. Eti sisi hatuna mvuto/motisha (incentive) wa kutosha kuwekeza katika vitu vinavyoleta maendeleo (development). Anasema hata kwenye kutoa elimu tunawekeza ki-supply na sio ki-demand ndio maana matokeo ni duni.
*Msome mchumi huyo kwenye makala hii: Douglas Rimmer on Learning about economic development from Africa.