Mdadisi ameguswa sana na ripoti maalum ya mwandishi wa habari, Daniel Mbega, ambaye ameifuta vumbi ripoti ya utafiti kuhusu migogoro ya yaliyokuwa mashamba ya NAFCO. Japokuwa kabrasha hilo limeandikwa kwa Kiingereza, mwandishi-mchunguzi huyu amefikisha ujumbe wake kwa Kiswahili tena kwa namna inayoweza kueleweka kirahisi. Fuatilia mfululizo wa uchambuzi wake katika viunganishi vifuatavyo:

http://www.kwanzajamii.com/?p=4557

http://www.mjengwablog.com/2012/11/mgogoro-wa-ardhi-kapunga-8.html

http://kilimohai.wordpress.com/2012/11/21/mapato-yalikuwa-makubwa-lakini-wakaubinafsisha-mradi/

Wanaeleza katika ripoti yao ya The state of Nafco farms (Hali ya mashamba ya Nafco), kwamba, uuzaji wa Shamba la Nafco Kapunga ulikwenda sambamba na uuzaji wa Shamba la Mbarali ambalo tangu mwaka 1977 Nafco ilipolichukua kwa Wachina lilitambulika kuwa na ukubwa wa hekta 5,575, lakini lilipouzwa ikaelezwa kwamba lina ukubwa wa hekta 5,842, ikiwa ni ongezeko la hekta 267 ambazo hazijulikani zilikotokea” – Daniel Mbega