TUTASHUGHULIKIA MATOKEO TU HADI LINI?

Sijasoma yote
yaliyoandikwa katika mjadala huu wa Wanabidii lakini nina
 machache
ya kuchangia kuhusu suala la Ikwiriri kwa kuwa ni eneo ambalo
 nimekuwa
nikifanya kazi za utafiti kwa muda mrefu sasa.


Takriban miaka
mitano mpaka kumi iliyopita hakukuwa na mfugaji wa
ng’ombe hata mmoja. Wengi wa
wafugaji ni wa kabila la wasukuma ambao
 wamehamia toka Ihefu. Tukumbuke
serikali iliwafukuza/kuwahamisha Ihefu 
kinyume cha taratibu na kuwanyang’anya
mifugo baadhi yao waliochelewa 
kuondoka. Walitakiwa kwenda maeneo tengefu ya
Lindi na Mtwara na kwingineko. Maeneo tengefu mengi hayafai kwa ufugaji kwani hayakutengwa
kwa kuzingatia mahitaji ya wafugaji: maji, malisho na
huduma za kijamii. Hivyo
wafugaji wamelazimika kubuni mbinu zao za
kuweza ku-survive in the absence of effective structural,
infrastructural and
institutional support systems from the State
.



Hali ikoje:
 Kwa
kuwa hakuna kanuni nzuri za kuhakikisha kuishi kwa pamoja baina ya 
wakulima na
wafugaji na kwa kuwa shughuli zao haziendani, kwa maana ya
 kwamba wanyama wa
wafugaji wanaharibu mazao ya wakulima, hitilafu
 zilipotokea, wananchi (wakulima
na wafugaji) walikimbilia ofisi za
 serikali za vijiji na polisi kuweza kupata
usuluhishi. Kesi 
ziliongezeka mno. Polisi wetu na viongozi wetu wa vijiji,
kata, tarafa
 na wilaya tunafahamu kuwa hawalipwi vizuri na serikali. Wafugaji
ambao 
huwa wana uwezo bora kimaisha na kifedha kuliko wakulima katika maeneo ya 
Ikwiriri
walianzisha mchezo mchafu wa kuhonga polisi na kuwabambikia
 kesi wakulima kuwa
wao ndio wavurugao amani.



Nina mifano
kadhaa kutoka kwa wananchi wengi niliopata kuongea nao.
 Mfano: Mzee XX amekuta
mifugo shambani kwake na kuanza kujibizana na
 mfugaji YY kufikia hatua ya
kutaka kupigana. Mkulima XX anatamka kuwa
 ni lazima suala hili alifikishe
kunakohusika. Mfugaji YY anachukua
 pikipiki na kuwahi Ikwiriri police post.
Mkulima XX anafika polisi,
anakamatwa kuwa ametishia uhai wa Mfugaji YY na
mifugo yake. Anawekwa
 ndani kwa muda ambao polisi wameamua wenyewe.



Nikitumia
taarifa halisi ambazo si rasmi kwa kuwa hazijatolewa na
vyombo vya usalama
(polisi) lakini nimezipata toka kwa jamaa zangu
waishio Ikwiriri:


Mapigano ya
juzi ni kilele cha ugomvi ambao umekuwa ukiendelea kwa
 miaka kadhaa sasa na
wakulima ndio wamekuwa waathirika wakubwa. Huyu
 Mzee alieuawa Ijumaa aliwahi
kutoa taarifa kuhusu wafugaji kuingiza
 mifugo shambani kwake mwaka jana.
Alikamatwa na kuwekwa ndani. 
Alipotoka aliendelea kudai haki yake kwa kwenda
mahakamani. Alishinda 
kesi mahakamani na mfugaji mhusika alitakiwa kuondosha
mifugo yake 
mara moja. Lakini hakufanya hivyo kwa kuwa mahakama si yenye
kusimamia 
migogoro ya wakulima na wafugaji on
a daily basis but
ni polisi, hivyo
 mfugaji aliendelea kuhonga polisi.



Siku ya tukio,
mkulima mzee wa miaka 60 alikuta mifugo shambani kwake
 na kuanza kujibizana na
wenye mifugo. Wafugaji walipiga kelele na 
kuchukua marungu, mapanga na silaha
nyinginezo wakampiga mpaka kumuua 
yule mzee. Ina lillah wa in illaih rajiun! Wananchi wakaenda kutoa
 taarifa
polisi Ikwiriri. Kwa mujibu wa wananchi, hawakupendezwa na
 namna polisi
walivyolishughulikia suala hili. Waliona kuwa polisi
 wamechukulia kana kwamba
kimekufa kiji-mnyama tu kidogodogo na si
 binadamu tena wa miaka 60 ambaye
alishinda kesi mahakamani kuhusu
 mgogoro uliopelekea mauti yake. Wananchi
wakulima wakasema “enough is
enough”.



Wakazifunga
barabara za kutoka Lindi na Dar na kuanza kushambuliana na 
wafugaji. Kwa kuwa
wafugaji waliompiga na kumuua yule mzee ni wa
kabila la kisukuma, wakulima
walilenga kuwashambulia wasukuma
 irrespective
ya kuwa ni wafugaji ama la. Maduka, magari, nyumba na
 mali nyinginezo
zinazomilikiwa na wasukuma zimechomwa moto. Polisi
 mmoja wa kabila la kisukuma
amechomewa nyumba yake kubwa yenye
 wapangaji kadhaa kwani wananchi walimtuhumu
kuwa huwa anawasaidia
 wasukuma wenzake.


Wakulima wa
Ikwiriri nilioongea nao kwa simu wanahoji kwamba: kwa nini
 vyombo vya habari na
jeshi la polisi wametoa takwimu za wafugaji
 waliojeruhiwa na kuharibiwa mali
zao lakini hawajasema kuhusu WANANCHI
 WAKULIMA WA KABILA LA WANDENGEREKO WAWILI
WALIOUAWA KWA RISASI NA MFUGAJI
 WA KABILA LA KISUKUMA SIKU YA MACHAFUKO? Kwao
wao, wanadai kuwa hii
 bado inalenga kumkandamiza mkulima hasa wa kabila la
kindengereko (nimetaja makabila kwa kuwa wao walioniambia wamesisitiza katika
maandiko
 nifanye hivyo ili ichangie kuonesha ukandamizaji wa kabila la
 wandengereko.
Mimi si mndengereko wa silazimishwi kufanya wanavyotaka
 wao, bali nimeona
nifanye hivi kujibu hoja ya mmoja wa wachangiaji
 aliyehoji kwa nini ukabila
umekuwa “issue” katika suala
hili.)



Sasa hivi hali
bado ni mbaya kwani Wandengereko wamedai hawawezi
kuendelea kuishi kwa kuonewa
na wasukuma, hivyo wasukuma waondoke. Hii 
ndio hali halisi kwa vyanzo
nilivyoweza kuvifikia mimi.
Maswali ambayo yameulizwa kuwa
 wafugaji waende wapi
na ni nani mwenye haki zaidi ya ardhi, mkulima au 
mfugaji? Majibu yangu ni kama
ifuatavyo:

Serikali
ilipaswa itambue mahitaji ya wafugaji kama vile kutenga
maeneo yenye malisho na
maji ya kutosha na kuweka miundombinu ya
kukidhi mahitaji hayo. Namna ambavyo
serikali inaachia suala hili liwe baina ya 
wakulima na wafugaji ndicho chanzo
kikubwa cha migogoro. Vijiji vingi 
vya Ikwiriri, Lindi na Mtwara
vimeshurutishwa na serikali kutengeneza 
mipango ya matumizi bora ya ardhi ikiwemo
kutenga maeneo ya wafugaji.
 Wananchi hawa hawana uzoefu na ufugaji na hivyo
hawajui mahitaji
 maalum ya wafugaji. Kwa mfano, katika Kijiji cha Mavuji
wilayani Kilwa,
 wananchi wametenga eneo la malisho ambalo liko milimani ambao
mifugo
 haiwezi kutembea kwa urahisi. Mipango hii ya matumizi bora ya ardhi
 imetengenezwa
bila ushiriki wa wafugaji kwa kuwa hakukuwa na wafugaji
 katika vijiji husika.
Halmashauri za Wilaya husika zilikuwa na jukumu la
kuhakikisha kuwa mipango ya
matumizi ya ardhi iliyotengenezwa imekidhi
 vigezo vya kitaalam ili kuepusha
migogoro kama hii tunayoiona sasa.
 Kwa hali ilivyo sasa, tutegemee migogoro
mingi kama hii kuibuka.


Tutaendelea
kushughulikia matokeo mpaka lini ilihali vyanzo twavijua?


Mwandishi: Baruani Mshale

Picha: Maggid Mjengwa