Juzi nimekuta hifadhi ya lililokuwa gazeti la Jenga katika maktaba. Lilikuwa linatolewa na Shirika la Maendeleo la Taiga (National Development Corporation-NDC). Bahati mbaya sikuwa na kamera nzuri. Ila natarajia kwenda kupitia kwa kina magazeti hayo ambayo picha zake nyingi zinaonesha jinsi ambavyo tulikuwa na nia, sababu na hata uwezo wa kuendelea katika sekta ya viwanda na kilimo. Natanguliza picha hizi, zingine nitaziweka siku za usoni.

