Watanzania wanazidi kujumuika katika Twitter kujadili masuala mbalimbali!
Mijadala hiyo ina mvuto sana hasa ukizingatia kuwa viongozi wa kijamii, kibiashara na hata kisiasa wanajumuika. Wapo Wabunge (mf. @DocFaustine na @zittokabwe), Wakurugenzi wa Makampuni (mf. @iMashibe na @beyakuze), Wanazuoni (mf. @Mwanasosholojia na @Mwanafalsafa) , Wanamuziki (mf. @mwasitiJna @Profesa_Jay), Waandishi wa Habari (mf. @kabsjourno na @salvarweyemamu), Watangazaji (mf. @barbarahassan na @nyangorojs)Wanaharakati (mf. @Irenei2011 na @rakeshrajani), Asasi za Kiraia (mf. @Darajatz na @HakiElimu) Mawaziri (mf. @AnnaTibaijuka na @Mnyambi ) – na hata Rais wa Nchi na Mama wa Kwanza (@jmkikwete na @salmakikwete)!
Kwa sasa mijadala mikali inayoendelea ni pamoja na wa #udinitz na #mashoga. Jana kulikuwa na mjadala mkali sana kuhusu #DowansAward ambao bado unaendelea. Hivi karibuni pia kulikuwa na mjadala mkali kuhusu ajali ya meli Zanzibar #ZanzibarBoatAccident . Udadisi ilijiunga rasmi mwaka jana baada ya kusitasita kwa muda mrefu (rejea https://udadisi.com/2010/12/twittering-tanzanias-transinformation.html)!