SWALI LA KIZUSHI:
Je, Katiba ya Tanzania inaruhusu kitu kama hiki: http://www.eagleworldnews.com/2011/09/25/vladimir-putin-to-run-for-president/ ?
JIBU:
Kwa ufahamu wangu hili haliwezekani kwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ingawa linawezekana kwa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar. Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania iliacha lile neno muhimu “Consecutive” vipindi vya uraisi mtu anavyoruhusiwa kutawala.
Kuhusu uraisi katiba ya Jamhuri inasema a person cannot run for more than two terms wakati ile ya Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, kama zilivyo ya Urusi na nchi kadhaa nyingine inasema a person cannot run for more than two ‘consecutive’ terms. Na hapo ndipo tofauti ilipo. Kwa Zanzibar, kama ilivyo Urusi, waweza kugombea zaidi ya vipindi viwili mradi tu umpumzike kwa angalau kipindi kimoja hapo katikati. Lakini kwa Jamhuri hakuna namna unayoweza kugombea zaidi ya vipindi viwili, iwe mfululizo au vinginevyo.
Kwa hiyo jibu ni Hapana, Mkapa hawezi kugombea tena uraisi kama Putin kwa katiba ilivyo sasa, kama mchakato wa mabadiliko ya katika hautalibadili hilo.
CHANZO:
http://groups.yahoo.com/group/Wanazuoni/message/11473
PICHA:
https://udadisi.com/2010/05/kuna-mambo-rais-mstaafu-mkapa-huwa.html