Katika safari yangu ya Loliondo kwa Babu nilibahatika kupata kipande kikubwa cha magadi. Kipande hicho kilikuwa kinauzwa kwa Shilingi 500 kando kando ya Ziwa Natron na wenyeji wa maeneo hayo. Katika basi letu watu wengi tu walinunua vipande hivyo kwa ajili ya dawa na matumizi mengine.
Lakini miaka michache iliyopita nilihudhuria mjadala mkali katika Ukumbi wa Karimjee kuhusu mpango wa kujenga kiwanda cha kuchimba magadi hayo. Wenyeji wa maeneo hayo ambao inasemekana walifadhiliwa na wapigania haki za wanyama na wanamazingira waliongea kwa uchungu mkubwa kuwa kiwanda hicho kitaharibu mazalia ya ndege wazuri wa flamingo pamoja na kuathiri upatikanaji wa maji katika eneo hilo.
Hapo Karimjee alikuwepo pia mwanaharakati maarufu Rugemeleza Nshala aliyeichambua ripoti ya athari za mazingira na kijamii – Environmental and Social Impact Assessment (ESIA) – iliyowasilishwa hapo kwa hisia kali ya kizalendo. Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) ilibidi likubali hoja hizo za wapinzani wa mradi huo japo wawakilishi wa wawekezaji nao waliongea kwa uchungu kuhusu jinsi ambavyo Tanzania inapata shida kuagiza magadi nje ya nchi ilhali ina magadi mengi sana hapo ziwani Natron. 

Je, ni lazima tuyachimbe magadi hayo kiwekezaji? Au tuwaachie tu wenyeji waendelee kufaidika nayo angalau kidogo kwa kuyauza kwa shilingi 500 kwa wasafiri wanaopita njia hiyo bila kuathiri vyanzo vya maji na mazalia ya flamingo? Na, je, wanyama wa Serengeti na ndege wa Natron ni kisingizio tosha cha kuwanyima wakazi wa Mto wa Mbu, Engaruka, Ngarasero, Ol Doinyo Lengai na maeneo mengine barabara ya lami walau inayofika Loliondo?

wanyama wa Serengeti na ndege wa Natron ni kisingizio tosha cha kuwanyima wakazi wa Mto wa Mbu, Engaruka, Ngarasero, Ol Doinyo Lengai na maeneo mengine barabara ya lami walau inayofika Loliondo?
Kinachotakiwa ni kuunganisha Mugumu na Musoma kwa lami na Loliondo iunganishwe na Arusha.
Ni muhimu vilevile kuangalia which area we are earning more kwa sasa na kulipa uzito unaostahili.