Hatimaye John Mnyikaametangazwa Mshindi wa Ubunge katika Jimbo la Ubungo. Matokeo yalicheleweshwa kutangazwa kupita kiasi bila sababu ya msingi. Wadau wa mgombea huyu walikesha juzi na jana usiku kuhakikisha kura hazichakachuliwi hasa ukizingatia kulikuwa na madai ya kufanyika kwa kitendo hicho katika uchaguzi wa 2005. Juhudi zao zimezaa matunda 2010.