
Sambamba na kuwafuata vijana walipo, asasi pia imezindua blogu yahttp://www.kijanakurayako2010.wordpress.com/ na kundi katika mtandao wa kijamii wa Facebook kwa jina la “Kuelekea Uchaguzi Mkuu 2010”.
Mradi huu ni wa kujitolea, unaendeshwa na vijana wenyewe pasi ufadhili wa wahisani ama shirika lolote. Lakini, inashirikiana na mashirika yaliyotoa machapisho ya Elimu ya Mpiga Kura kusambaza kwa vijana.
Tunawahamasisha vijana wote watembelee mitandao na kuchangia kwa habari, picha n.k.
Kijana Jitokeze Kupiga Kura 2010!
Frederick Fussi,
Katibu Mtendaji -Tanzania Youth Vision Association