Ni jambo ka kupendeza tena la kuvutia sana kuona shule ya Msingi hii katika Kijiji cha Maore huko Gonja katika Wilaya ya Same Mkoani Kilimanjaro ikiwa na michoro ya wazi yenye kutoa elimu kwa wanafunzi na jamii kwa ujumla. Mdadisi wetu anajiuliza inakuwaje ujumbe ulio katika michoro hiyo unakuwa kwa lugha, historia na hata majina ya kigeni? Je, mtoto aliyezaliwa na kukulia katika kijiji ambacho shule hiyo ipo anawezaje kuoanisha kwa urahisi historia ya familia yake na historia ya familia ya ‘Dakta Siagiuwanja’ na mkewe ‘WaridiMaria’?