Kwa mujibuwa Vyombo vya HabariMheshimiwa Waziri Mkuu, ametatua mgogoro uliopelekea wafanyakazi wa Shirika la Reli lililobinafsishwa kwa kampuni kutoka India Kugoma. Sio siri ni jambo la kufurahisha kuona kuwa wafanyakazi hao watalipwa mishahara yao. Ila swali la kujiuliza ni iweje mwekezaji ashindwe kuhudumia wafanyakazi wake mpaka Serikali imkope shilingi bilioni 3.6? Yaani ule uwezeshaji wote wa vivutio wanavyopewa na TIC havitoshi?

Na hizo dalili za wingu la ufisadiambazo zinajidhihirisha zitachunguzwa au yaliyopita si ndwele tugange yajayo? Naam yajayo yatatokea baada ya hiyo miezi 5 ambapo hizo bilioni 3.6 zitakuwa zimekwisha. Je, mwekezaji atakuwa amejizatiti au atataka kuwezeshwa tena na Serikali yetu iliyoelemewa na mizigo mingi ya madeni ya uwekezaji mbovu na inayowezeshwa na wafadhili?

Hakika ndio maana Mwalimu Nyerere alilalamika kuwa mbona wanatuambia tubinafsishe vya kwetu wakati vyao hawabinafsishi. Ndio maana alisisitiza kuwa ‘you cannot nationalize nothing’ yaani huwezi kubinafsisha kisichopo. Kumbe tulikuwa navyo na fedha tunazo. Kuifadhili TRL kunadhihirisha kuwa bongo tambarare kama anavyouliza kwa bezo mtoa maoni wa blogu ya Michuzi?