Harakati za wanawake kweli zimeanzia mbali!Hili ndio toleo la kwanza la Sauti ya Siti!Humo ndani lina mada motomoto ambazo zinaonyesha jinsi gani wanaharakati walivyokuwa na ari ya kupigania haki za wanawake!

Mapambano bado yanaendelea! Siku ya Wanawake Duniani ni sehemu tu ya mapambano haya! Je, wewe ni sehemu ya vuguvugu hili? Unauchochea moto huu au unaupooza? Je, unashiriki katika kuipaza Sauti ya Siti au unaikwaza?