
Je, maji haya hayatumiki kwa kuwa hatuna uwezo wa kujenga mitambo?Au hayatumiki kwa sababu hayana nguvukasi ya kutosha kutoa kiwango cha kutosha cha umeme? ‘Kwa nini?’
Kuna umuhimu wa kuendelea kudadisi maana bei ya umeme inazidi kupanda. Nasikia mwezi huu imepanda kwa zaidi ya 20% japokuwa nishati hii inafikia takribani 10% tu ya wananchi!Umeme ni bidhaa adimu Tanzania, Afrika Kusini, Zambia, Zimbabwe n.k, kwa nini hatuuzalishi kwa wingi?
Mimi bado natatizwa na mantiki ya Serikali kuachana na mradi wa Stiegler’s Gorge. Kwa wasiojua habari ya mradi huu kuna dondoo chache katika http://www.bongotz.com/bongoyetu10_%2029_06.htm