
“Ole wake kiongozi mzembe na asiye na nidhamu nitakayemkuta: Kiongozi wa siasa hana usalama wa aina yoyote. Usalama wake ni kudra ya Mungu na Wananchi peke yake. Viongozi wazembe na wabadhirifu wahesabu siku zao. Labda tusiwajue. Hawa hatuna sababu ya kuwapa imani, kuwa tutawalinda kama vitendo vyao viovu” – Edward Moringe Sokoine, 26 Machi 1983
“Juu ya suala hili la mapato kutolingana na matumizi ni kwamba tungependa kupunguza uongezaji wa wataalam wasiohitajika katika Serikali na katika mashirika ya umma mpaka hapo hali yetu ya uchumi itakapokuwa katika hali nzuri” – Edward Moringe Sokoine, 23 Oktoba 1982
“Serikali inasimamia bei, lakini Serikali yetu itakwenda mpaka itasimamia bei ya mhogo, dagaa na bei ya kila kitu? Haiwezekani, vitu vingine ni lazima vizalishwe kwa wingi ili bei yenyewe iweze kujirekebisha” – Edward Moringe Sokoine, 24 Septemba 1983
“Wajibu wa kila Mtanzania, kila familia na kila anayekula ni kujilisha mwenyewe. Si wajibu wa Taifa kumlisha mtu. Unaweza ukasaidiwa unapopatikana na janga. Lakini kama hakuna janga ni wajibu wa kila mtu aweze kujitosheleza kwa chakula na atoe ziada kwa Taifa” – Edward Moringe Sokoine, 4 Oktoba 1983
“Vijana leo wengi wana mali zaidi kuliko wazee waliofanya kazi miaka thelathini hadi arobaini. Lakini wanaitaka Serikali ndiyo iwaulize mali hiyo wameipata wapi. Hivi kwa nini mzazi asimuulize mwanae, ‘mali hii umeipata wapi?'” – Edward Moringe Sokoine, 23 Oktoba 1983
“Katika nchi inayojali haki na usawa, majeshi hayana budi yawe ni chombo cha kulinda haki na maslahi ya walio wengi. Na kamwe hayaruhusiwi kuwa ni chombo cha wachache wenye kujali nafsi zao na kusahau maslahi ya walio wengi” – Edward Moringe Sokoine, 1Februari 1977

alikuwa mtu wa MUNGU aliyeletwa kusaidia watu wa MUNGU.
Kwa maneno aliyosema hapo juu alishajiweka hatarini
Jamaa hakika alikuwa ndiye rais tuliyemhitaji sana, tena nyakati hizi
Alikuwa mkweli mpenda haki hakuwa kigeugeu kama mnafiki na woga aliutupa pembeni sana.
itachukua muda sana kupata viongozi waadilifu kama EDWARD MORINGE SOKOINE!
Never shall we get such a person!
Hao ni viumbe ambao walikuja kwa wakati maalum haitowezekana kuwapata watu kama hao
Kwa hakika Tanzania ya leo inahitaji kiongozi mwenye uthubutu.
Kwa hakika Tanzania ya leo inahitaji kiongozi mwenye uthubutu.
alikuwa na kauli nzito sana…sasa hivi hazipo tena
Ndivyo ilivyo Mtu mzuri hawezi kuishi muda mrefu.
Soma maandiko haya; Zaburi 146:3-5
Hahaha mungu mlaze pema
Mungu amlaze pema
Moringe ndio magufuri Wa Leo mwendo Wa magufuli ndio nyayo za marehemu Edward sokoine
Mimi nadhani tufike mahali tuelewane kwamba, nchi haitakiwi kuongozwa kwa akili za mtu binafsi, bali, tufuate misingi ya Katiba ambayo ndiyo sheria mama. Nchi ni kama chombo kilicho hai na kina mfumo kamili wa uhai wake.Kama chombo kinatumia petroli, kila rubani anayekabidhiwa atumie petroli asiweke ubunifu wake binafsi la sivyo injini ambayo watu wengi waliisha ikubali yaani (KATIBA) haitakuwa na maana. Kuibuka kwa viongozi mashujaa ni tafsiri kuwa watangulizi walilegeza mambo fulanifulani katika mfumo wa chombo.
Hakika alikuwa kiongozi wa watu.lakini Mungu hajatuacha wakiwa kwa kutupatia Magufuli.
Magufuli hana mfano wake. Mungu amejibu maombi ya watanzania na waafrika kwa ujimla wetu.
Sokoine kafufukia chato…asante mungu