“….Licha ya juhudi hizo bado Ardhi ni tatizo kubwa kwa wananchi wa Meru…Hivi Leo Ardhi kubwa ya Meru imeshikwa na matajiri na kulimwa Maua. Kilimo hiki cha Maua mwaka 2008 kiliingizia Taifa fedha za kigeni takribani tshs 150bn. Hata hivyo kuna malalamiko makubwa sana ya wananchi wanaofanya kazi katika mashamba haya kuhusu malipo duni na nyenzo za kufanyia kazi. Kuna malalamiko kuhusu kemikali na madawa yanayotumika na afya ya mfanyakazi kutozingatiwa….Haya ndio yanajenga hasira ya wananchi wa Meru. Hasira hii kwa vyovyote itahamishiwa katika sanduku la kura ili kumpata Mbunge kutoka miongoni mwao atakayeweza kusimama kidete kuhakikisha Ardhi inapatikana kwa wananchi wa Meru….” –


Zitto Kabwe


Ardhi, Maji na Ajira kuamua Ubunge Arumeru Mashariki

http://zittokabwe.wordpress.com/2012/03/11/ardhi-maji-na-ajira-kuamua-ubunge-arumeru-mashariki/