Loading Events

#LadhaZaUani  #UtabibuUani

Soma book Cafe kwa kushirikiana na wasanii wanakualika kushiriki katika shughuli uliyobeba maudhui ya Uani. Uani ni nafasi ya kijadi, waliyotengewa wanawake kujisitiri. Kuna kanuni na taratibu zilizowekwa ili kuhakikisha kuwa, wale wanaozitumia nafasi hizo wanazingatia maadili ya mfumo dume. Nia ya kuratibu hafla hii tunayoiita Uani ni kuhoji kanuni hizi na mitazamo hasi juu ya sehemu hii muhimu. Tunataka kupanua wigo wa nafasi hizi ili ziweze kuwakumbatia wana na binti wa kizazi hiki. Pamoja na hayo, tunataka kuchota hazina ya maarifa na historia iliyohifadhiwa humo, ili tusifanye kosa la kutupa mwana na maji ya moto. Hafla hii inafungua wigo mpana katika maeneo matatu, maarifa, utabibu na ladha za uani.

Utabibu kutoka Uani:Maarifa ya jinsi gani vitu mbalimbali kama miti shamba,manukato na viungo asili, kusinga na kukanda mwili kama mbinu baadhi zilizotumiwa na wanawake uani katika kuponya mwili na kujiburudisha.

Ladha za uani; Tunapenda kukukaribisha wewe kuonja chakula cha asili; kuhoji utunzaji wa vyakula; utunzaji wake; kusikiliza hadhithi, mila na desturi, miiko ya maandalizi yake.

Leave A Comment

Go to Top