Mbinu ya Kuzuia au Kupunguza Wimbi la Msongamano wa Wagonjwa wengi kwa Mkupuo wenye Virusi vya Corona
Udadisi inakuletea mfululizo wa makala, michoro, video, na katuni kwa lugha ya Kiswahili za kuielezea kwa urahisi mbinu ijulikanayo kwa Kiingereza kama ‘Flatten the Curve’ au ‘Flattening the Curve.’ Udadisi inaamini pengine hii ndiyo dhana ambayo pia ni mbinu muhimu kuliko zote inayoweza kutusaidia katika kupambana na janga la kirusi cha corona na ugonjwa wa COVID-19 unaoendelea kusambaa kwa kasi sana duniani.
Kwa tafsiri rahisi, #FlattenTheCurve au #FlatteningTheCurve ni dhana na mbinu inayosaidia kupunguza kasi ya kuenea kwa ugonjwa huo kwa kuhakikisha unapunguza wimbi kubwa la wingi wa wagonjwa kwa mkupuo unaopelekea hospitali, zahanati na vituo mbalimbali vya afya kuelemewa na msongamano wa wagonjwa wanaohitaji huduma hiyo. Upunguaji huo huwezesha taasisi hizo za kutoa huduma za afya pamoja na sekta nzima ya afya ziweze kumudu kuhudumia wagonjwa na hivyo kupelekea kupungua kwa wingi wa wagonjwa na maambukizi katika jamii kwa ujumla.
Ahsante sana kwa kuchukua wajibu wa kuihabarisha jamii.