Kwa wale mnaofuatilia harakati za kudai haki kupitia migomo mtakubaliana nami kuwa sakata la walimu kuwapiga mawe viongozi wao jana baada ya viongozi hao kutoa tamko la kusitisha mgomo ni la aina yake. Tamko hilo la uongozi wa chama cha walimu lilifuatia tamko la mahakama kuzuia mgomo huo uliokuwa uanze leo. Walimu waliokuwa wamepandwa na hasira/jazba walichukua sheria mkononi na kuna kila dalili kuwa kama vyombo vya dola/sheria visingeingilia kati basi hata uhai ungeweza kutolewa. Ikumbukwe kuwa hivi karibuni wafanyakazi wa benki ijulikanayo kama NMB walilazimika kukubali kuwa sheria ni msumeno kwa kusitisha mgomo wao baada ya ‘agizo’ la mahakama.
