Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Mashirika ya Umma ameandika barua ya wazi kwa Mjumbe ‘mpya’ na mwenye ushawishi mkubwa wa kampuni inayojiita African Barrick Gold (ABG). Barua hiyo ambayo bahati mbaya au nzuri imeandikwa kwa lugha ya Kiingereza inapatikana hapa http://zittokabwe.wordpress.com/2011/12/02/an-open-letter-to-balozi-mwapachu-on-abg-crosslisting/ . Mjumbe huyo wa bodi anajiandaa kuijibu kwa kina barua hiyo. Ni matumaini ya Udadisi kuwa mjadala huu wa vinara wa sekta ya madini utatafsiriwa kwa Kiswahili na kusomwa na Watanzania wengi tunaojiuliza: Kulikoni Utajiri wote huo wa Madini Tanzania bado Nchi i Maskini?