Mwanamuziki mashuhuri, Dkt Remmy Ongala, ametutoka kimwili jana usiku. Atakumbukwa kwa nyimbo zake zenye ujumbe muhimu kuhusu maisha haya mafupi ya mwanadamu. Vibao hivyo ni pamoja na ‘Kifo’; ‘Kipenda Roho’; ‘Mtaka Yote’; na ‘Mama Nalia’. Baada ya kubatizwa na Kanisa la Waadventista Wasabato aliimba nyimbo za Injili vile vile.
“kifo, kifo
siku yangu ikifika eeh
kifo niarifu mapema
niage wanangu
niage familia yangu yote
pesa zangu nizigawanye
zimebaki nizile mwenyewe
kifo nakusubiri kwa hamu“
– Dkt Remmy Ongala