“Tarehe 20 Januari 1964 maofisa 15 wa Jeshi la Tanganyika (Tanganyika Army) lililorithiwa kutoka serikali ya kikoloni ya Tanganyika, Colito Barracks (Kambi ya Lugalo) waliongoza maasi ya kijeshi dhidi ya serikali ya Tanganyika. Kikundi kimoja kilikwenda Ikulu kutaka kumlazimisha Rais Nyerere kukubali matakwa yao. Haijulikani ingekuwaje kama kingefanikiwa, na kama Rais Nyerere angeyakataa madai yake. Lolote lingetokea na historia ya Tanzania na ya Afrika ingeathirika vibaya mno. Kwa ujasiri na ubunifu makini, Peter Bwimbo, aliyekuwa mkuu wa kitengo cha ulinzi wa viongozi, (Presidential Securty Unit) na mlinzi mkuu (Body Guard) wa Rais Nyerere, iliwahamisha Rais Nyerere na Makamo wake Rashis Kawawa, akawapeleka mahali salama, akawaepusha na hatari, pengine ya kuuawa. Hiyo ndiyo iliyoitwa Operesheni Magogoni. Katika kitabu hiki, Mzee Peter Bwimbo, kwa maelezo yake mwenyewe ametoa siri ambayo ni wachache sana waliyoifahamu; haya ndiyo maelezo sahihi ya mbinu alizotumia kuwaokoa viongozi wa nchi” –

http://www.africanbookscollective.com/books/peter-dm-bwimbo-mlinzi-mkuu-wa-mwalimu-nyerere

NB: Kisome kwenye Vitabu Vya Google

  1. Unknown September 15, 2016 at 11:02 am

    kwanza nikupongeze mtunzi wa kitabu hiki kwa kuchukua mufa wako na kutafuta masalia ya historia ya mlinzi huyu makini sana.peter DM bwimbo hakika ni shujaaa na mlinzi Makini sana wakati wa utawala wa mwalimu Julius k nyerere . vitabu kama hivi vinafaa kuwekwa mashuleni ili wanafunzi wajifunze uzalendo na taifa lao pia makumbusho ya taifa vinafaaa kuwekwa pia watu wapate kujua maaana kuna wengi sana hawajui historia hii nzuri

  2. Unknown September 15, 2016 at 11:04 am

Comments are closed.