Na Jasper “Kido” (@KidoJapa)
Nani asiyependa mawingu kuyakata?Nani mabawa akipataangani hatoruka?Ni wivu bila shaka na kijiba cha ukata,Mawaa yamewajaaWasokheri washupaa,Nao ‘tasema kutwawakichoka wataacha,
Wakorome kama churanami tembo sitoufyata,Nayo maji nitakunywana sitojali vibaraka,Mchanga n’nalambaKwa Jamhuri naapa,Magharibi nitakwendaMashariki kadhalika,Kusi, kasi nitafikaBaraka kuzichota,
Ya wahenga yashapitaHizi ni mpya kurasa,Zama kale si sasaMambo yapaswa badilika,Kweli kizuri chajiuzaIla chapaswa pia jitembeza,Wala si Singida au KilosaBali Saudia na Ibiza,Katikati ya chochoro za Ulaya na AmerikaHuko ndipo yapaswa katiza,Ziso haya ingia tokaNdizo watakazo zikumbuka,
Achaneni na wanaobezaHawayajui ya wakubwa,Lini walishika madarakaNdio waweze kutufunza,Tuwachunge yatupasaHawana nia ya dhati kwa hakika,Tena tunapaswa jiuliza…Ipi dhamira yao, nchi yetu ‘kibaki nyuma?Ni vipi wao wataweza faidika?Ni kipi haswa wa’tuficha?Si watu wema hawaNi wabaya na wanyama bila shaka,
Watafura na kusemana matusi kunivika,Hata nyimbo watatungana makala kuandika,Sitojali, matope ‘kinipakaWangu Mola atalipa,Ooh Ya Rabi JaliaTiketi ninapokwenda kuikata,Uwe Rubani muongoza njiaNiendapo kuyasaka mapesa,Kituo kinachofuata…ni kwenye visima vya mafuta.
Comments are closed.

Kaka Kido. Hongera sana kiswahili kimetulia sana. Maelezo yamenyooka
Shukrani sana Kaka.
Ni shairi nzuri sana, limenipa hisia za kimapinduzi
Hongera mwanaharakati
Asante sana. Nimefarijika kusikia limeibua hisia njema kwako.
Wow…great!!
:)
Shairi zuri sana nimelipenda, nikama mshairi amechukua mawazo yangu yakila siku na kuwasilisha kwa ushairi mnono.
Erick, nimefarijika sana kuwa nimeweza kushughulika na kiu yako na kuweza kuyaweka mawazo yako katika kazi hii. Asante sana.
🦍
nzuri sana
Asante sana