Yarabi huu mwaka na uishe, uishe na shari zake. Mwaka gani huu uliojaa chuki, maumivu, uzandiki, udhalimu, fitna na kila aina ya dhulma? Yailai, mwaka huu nimepata wahaka wa roho, dhoruba ya nafsi na gagasuko la akili. Ama kweli walijisemea wazigua “Mwaka wako humpi mwenzako” !
Hakika huu ulikuwa mwaka wangu, kila janga lililotakiwa kutokea lilitokea.Ila Alhamdulillah nimekuzwa kuamini kuwa lisiloniua litanitia adabu, si haba nimeshika adabu yangu, tena mkononi. Nimewajua walimwengu kwa mapana na marefu, ama kweli viumbe wazito.
Haiyumkini kwenye kila kubwa kuna kubwa zaidi, rafiki yangu mie, tena hatukukutana barabarani, wa miaka nenda rudi, hatukuwa mashost wa kupigiana simu kila dakika na kuulizana hali kila saa ila najua yeye alikuwa mtu wangu, wa usongani, wa mabuku na faraja, leo hii kaninunia only God’s knows why, as if I don’t have enough problems already – huu mwaka huu, hakuna rangi sijaona walai.
Natamani ningekuwa na uwezo wa kumpotezea, ila siwezi jamani, naumia. Labda kinachoniumiza zaidi ni kutojua what happened! Najiuliza nimemkosea kikubwa kipi mpaka akanichunia to that extent? Namjua ni mwingi wa staha, busara, uvumilivu na asiyependa makuu, sasa mpaka imefikia hatua ya kuni-delete mazima bila hata kunipa haki yangu ya kujieleza lazima nimemuumiza vibaya na naumia kwa kutokujua ni nini hasa nilichofanya. Natamani angeniambia, nikajua, nikajifunza na nikatubu, lakini wapi, nimeachwa nalo jaramba la mwahako nihangaike nalo.
Kibinadamu niliamini ananiamini, anajua what am capable of and what am not, labda naumia kwa kuwa sijawahi kuwa na dhamira ya kukutendea baya, labda naumia kwa kuwa, I honestly care na labla naumia kwa kuwa sikutarajia hili kutokea, of all people! Not you rafiki.
Najua sina njia tena ya kukwambia ninayotaka kukwambia, matumaini yangu pekee ni kuwa huu waraka utakufikia. Nikuhakikishie tu naheshimu mawazo na maamuzi yako, najua kila chenye mwanzo hakikosi kuwa na mwisho labda huu ndio mwisho wetu. Wanasema wenye busara zao, kuwa muda mwingine kumuachia aende ndiyo mapenzi makuu na la kuvunda halina ubani.
Rafiki yangu niliyekupenda, nenda tu… japo nafsi yangu i dhoofu lhali, nikikumbuka how you made me better as a person and writer.
2019, nimekuchoka, 2020 uwe na ahueni tafadhali.