“Nilipoanza kusoma Sudi ya Yohana, nilijua jambo moja — ninataka kusoma kila kitabu alichokiandika Chachage. Katika uhai wake, aliandika riwaya nne ikiwemo Sudi ya Yohana (1981), Kivuli (1984), Almasi za Bandia (1990) na Makuadi wa Soko Huria (2002). Nilifurahi kufahamu kuwa kitabu hiki kilipochapishwa, Chachage alikuwa na umri wa miaka 26 na mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. Jambo hili lilinifurahisha sana. Unaposoma kitabu hiki, unaona jinsi gani alikuwa kijana mwenye upeo mkubwa, akichokoza mawazo kwa uandishi wake na kuchochea mapinduzi ya kifikra. Hiki ni kitabu kidogo, lakini kimesheheni. Sio kitabu cha hovyohovyo” – https://medium.com/@Es_Taa/sudi-ya-yohana-na-c-s-l-chachage-24e8b329f006