Salaam wadau wa elimu Tanzania -amani na iwe nanyi! Sijaona jipya kwenye Matokeo ya Mtihani wa Taifa wa Kidato cha 4 yaliyotangazwa juzi – kufeli bado kunaongezeka tu! Sioni jipya pia katika mijadala na malalamiko achilia mbali maazimio na mipango yetu ya kuinusuru sekta hiimahututi – ni yale yale tu! Sidhani kama nitakuwa mbali na ukweli nikisema kuwa tumeshaikatia tamaa elimu – tumeiacha iende zake kaburini! Sasa tumekubali yaishe na ndio hivyo tupo kwenye hitma ya kifo cha kifikra na kimaarifa cha kizazi hiki – naam kizazi cha kijinga!