Wazungumzaji Wakisikilizana

(Kutoka Kushoto: Fancy Nkuhi, Zitto Kabwe na Omar Ilyas)

Washiriki wakifuatilia Mazungumzo

Wadau wakijumuika katika Iftar

——————————————

Mfululizo wa Mazungumzo ya Tanzania Njema umeanza rasmi Jumapili iliyopita. Mazungumzo haya yanaratibiwa na Taasisi ya Tanzanianjema. Washiriki mbalimbali hususan vijana walijumuika pamoja siku hiyo katika Mkahawa wa Vitabu wa Somakuzungumza na wanasiasa vijana kuhusu changamoto wanazozipata katika medani ya siasa na hasa katika harakati zinazoendelea za uchaguzi. Wanasiasa waliotoa uzoefu wao ni Fancy Nkuhi, aliyekuwa katika kampeni za kupata nafasi ya kugombea ubunge kwa tiketi ya CCM/UVCCM, na Zitto Kabweambaye anagombea tena nafasi ya Ubunge katika Jimbo la Kigoma Kaskazini kwa tiketi ya CHADEMA. Mfululuzo wa mazungumzo haya utaendelea, kwa taarifa zaidi tembeleahttp://www.tanzanianjema.com/