Na Zuhura Yunus (@venusnyota)
NAWAZA kwa nini baadhi ya nchi za AFRIKA zinaona tabu kufanya LOCKDOWN au hata PARTIAL LOCKDOWN katika kupambana na janga la COVID-19?
NAWAZA inakuwaje baadhi ya nchi nyingine za kimagharibi na hata za Afrika Mashariki na Kati zimefanikiwa vipi kukabiliana na janga hili hata wasiwe na kifo hata kimoja.
NAWAZA iwapo mabasi ya masafa marefu, yaani mikoani yanaweza kuzuiwa ili kupunguza kasi ya kusambaza virusi vya korona.
NAWAZA kama safari za ndege za kuingia nchi za Afrika pamoja na safari zozote mipakani zisitishwe kwa muda mpaka nchi ziweze kudhibiti kusambaa kwa virusi vya korona.
NAWAZA kuhusu nchi zenye kutumia usafiri wa maji kusitisha safari hizo kwa muda.
NAWAZA kwani nikiswali nyumbani bila ya kwenda msikitini/kanisani dua yangu haitopokelewa?
NAWAZA hivi Mungu mwingi wa Rehema ataniadhibu au kunipa madhambi kwa sababu sijaenda kufanya maombi kwenye nyumba ya ibada na badala yake nikasali nyumbani?
NAWAZA ili watu wasikose rizki, hatuwezi kuwa wabunifu na kutumia bodaboda kununua vitu na kutuachia nje ya nyumba.
NAWAZA Hawawezi watu wakapanga foleni na kuingia mmoja mmoja madukani kuepusha kusambaa kwa virusi vya korona.
NAWAZA mama lishe, wauza vitafunio asubuhi kama vitumbua n.k, hawawezi kwenda kwenye maeneo yao kwa muda maalum na kwa zamu na kuondoka haraka baada tu ya kumaliza kuuza vyakula hivyo.
NAWAZA nchi za Afrika haziwezi kusitisha kudai bili za maji au angalau kupunguza gharama za kulipia.
NAWAZA wauza bidhaa masokoni hawawezi kukaa mita mbili baina ya muuzaji na muuzaji.
NAWAZA serikali hazina mifuko maalum ya maafa na dharura kuweza kugawa chakula kwa familia ambazo hazitoweza kumudu chakula wakati wa PARTIAL LOCKDOWN.
NAWAZA pesa za makusanyo ya kodi haziwezi kutumika kugawa kwa kila familia simu moja ya mkononi angalau wanafunzi waweze kudurusu kwa njia ya kidijitali.
NAWAZA mabadiliko na ubunifu muhimu hasa kununua vitu mtandaoni na kwa njia za simu.
NAWAZA kuna ubaya gani kujua takwimu za watu wote waliopimwa, walioathirika na kufa kutokana na virusi ili niweze kujikinga zaidi.
NAWAZA Mwana Mfalme na Waziri Mkuu wa Uingereza walijitangaza walipoathirika ila kuna usiri mkubwa miongoni mwa viongozi wa Afrika.
NAWAZA namna viongozi wanawake kama Anna Mghwira waliyvo na ujasiri wa kueleza hadharani kuhusumaambukizi waliyoyapata.
NAWAZA Hivi kwani ugonjwa huu wa COVID-19 ni wa aibu?
NAWAZA naendelea kuwaza…
Comments are closed.
Tunashukuru kwa kutukumbusha ila nchi zetu hazina uchungu na wananchi wao.kuna baadhi ya nchi zimefanya lockdown mimi nimezipenda sana na nikatamani nana hapa kwetu tz tuinge ila viongozi wa juu hawajachukua hatua na sijui nini sababu maana wanajali kiongiza kodi kuliko uhai wa mlipa kodi
Pole dada kwa mawazo ila kama ubaiwazia Tanzania utapata vidonda vya tumbo…. viongozi wetu wanajifikiria wenyewe tu
Hatuna uongozi Zuhura. Hasa Tanzania. Waliyoko madarakani ni watawala wasio na uongozi! Hiyo ndio shida kubwa tuliyonayo.
Yaani mi niseme unawaza kama mimi Zuhra..Lakini ni nani wa kunikisikiliza baada ya kuwaza?
Alexander Ndondeye, pole sana kwa Mawazo hayo maoni ya wengi nayaunga mkono, Bungeni watu wanakufa lakini et ni lazima Bunge liendelee… Linaendeleaje wakati wahusika wanakufa??
UDADISI wako umemaliza kila kitu jambo umesahau Nyungu yakujifukinza
Tupo km samaki ndani ya maji tunamawazo mazuri lkn hatuna mamlaka yakuamua iwe na ikawa…hvy ngojea tuendelee kusubiria maajabu ya Mungu mwenyewe.
Asante kwa mawazo yako mazuri lakini Mimi naona hayo mawazo yako ni Fact ambazo viongozi wetu wagechukua na kufanyia kazi.I am big fanatic of your articles keep drop those thoughts.
Kila nchi inautaratibu wake. Tanzania inataratibu za kuratibu nakupambana na majanga kama hayo. Hakuna cha kushangaa hapo
Kuna mambo kadha Wa kadha ambayo tunahitaji kujifunza hapo. Unadhani ukimuagiza bodaboda kwenda kununua yeye hawezi kuambukizwa covid 19? Vipi kununua bidhaa Kwa njia ya mtandao, unafikiri nchi yako inauwezo Wa kuwezesha mtandao ya robot transportation na hata drons kuwawasilishia bidhaa walio kwenye lockdown? Tujaribu kutoa hoja kuntu Kwa kufikiri mahali nchi yetu ilipo.