Mchakato huu wa kuzalisha mkaa utokanao na uchafu/takataka kwa kutumia mtambo uliotengenezwa hapa nchini ulinivutia sana katika maonyesho ya Saba Saba 2008. Mtambo huu umetengenezwa na taasisi ya teknolojia inayofaa kutumika vijijini (Appropriate Rural Technology Institute). Mwaka 2002 taasisi hii ya ARTI-TZilishinda Tuzo ya Nishati Endelevu ya Ashden. Jitihada zake za kuvumbua nishati mbadala zinazoendana na mazingira yetu ni kielelezo tosha kuwa uwezo/utaalamu wa kujifanyia mambo yetu wenyewe tunao. Hii ndio ilikuwa njozi ya Muasisi wa Siasa na Elimu ya Kujitegemea.

Hatua ya 1: Kukusanya Takataka
Hatua ya 2: Kuchoma Takataka

Hatua ya 3: Kufinyanga Mkaa
Hatua ya 4: Kutumia Mkaa


