Mkahawa wa
Vitabu Soma 
@SomaMkahawani uko mbioni kuanzisha
utaratibu wa kumfikishia mteja kitabu anachohitaji pale alipo. Utaratibu huo
umepangwa kuzinduliwa rasmi juma lijalo. Maadam Wanazuoni kadhaa wametangaza
nia ya kupata kitabu kipya cha Mwanazuoni mwenzetu Richard
Mabala kiitwacho 
Run Free kilichoshinda Tuzo ya BURT ya mwaka huu, Soma Book Cafe itafungua
pazia nacho.

Kama
unataka kufikishwa kitabu hicho mpaka ulipo (ofisini, chuoni au karibu na
mahala hapo), bei yake ni Tsh 10,500. Ila kama utaenda moja kwa moja
kukinunua mwenyewe kwenye duka la vitabu Soma (http://www.somabookcafe.com)
bei yake itakuwa ni Tsh 10,000.

Kama
unataka kufikishiwa kitabu ulipo tafadhali tuma barua pepe yenye anuani yako na
namba ya simu kwa: somabookcafe@yahoo.com

Wasalaam,

Timu Ya Vitabu Soma