TAFSIRI PICHA HII ILIYOPIGWA DODOMA HIVI KARIBUNI
Chambi Chachage2021-05-28T02:33:45+03:00
Assistant Professor and founder of @Udadisi/Profesa Msaidizi na Muasisi wa @Udadisi - https://udadisi.com/chambi-chachage/
Akaunti ya Twita/Twitter Handle: @ChambiChachage
Jibu la Mdau # 1:
Kwamba, Waziri Mkuu Pinda ni mdogo kwa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, jambo ambalo ni ujinga mtupu.
Kwamba, haijulikani ni wakati gani itifaki ya chama inafuatwa na ni wakati gani ya serikali inafuatwa.
Spika wa Bunge ni sehemu ya CCM kwa hiyo ndiyo maana hakuna haki bungeni.
Lowassa ataumizwa.
Jibu la Mdau # 2:
Nilipoangalia mara ya kwanza nikasema labda these guys are reading too much into this. Lakini kuiangalia tena nikasema kila mtu amekaa hapa kwa sababu ni kiongozi wa juu wa chama au serikali. Lakini Mheshimiwa Lowassa sikuweza kuamua hapa kwamba yuko katika hii inner cirle in what capacity. Kama Ubunge, kuna wabunge wengine weeeeeeengi ambao hawako hapa, Kama ni Uwaziri Mkuu Mstaafu, kuna wenzake wengi ambao pia wangekuwepo. Ila nikajifariji kwamba labda yupo hapa kwa sababu ndiye waziri mkuu mstaafu pekee ambaye bado ni mbunge.