By Fadhy Mtanga (@FadhyMtanga)
Alizaliwa mwanamke
Akitambulishwa kwa rangi
Akipigania ukombozi
Kwenye kitovu cha Soweto
Alikunyanzwa na ubaguzi wa rangi
Uliotendwa nyakati za mwambwo
Kuanzia Kroonstad
Hadi Sharpville
Mama wa taifa
Binti wa watu
Dada wa Afrika yote
Shujaa wa mapambano
Watu wako watatawala
Ardhi na migodi
Hadi chini kabisa Marikana
Na hata katikati ya mbuga
Kwa heri Mama Winnie
Mtoto wa hii ardhi
Mkuki wa taifa
Roho ya Afrika Kusini
26.03.2020.