Hivi tangazo
linaloonesha mwalimu anafundisha halafu mwanafunzi anashangilia kupata ujumbe
wa simu linatuma ujumbe gani kwa jamii?

DAN:

Wanafunzi (hasa
wa sekondari na vyuo) ni kundi linalogombaniwa sana na makampuni ya
simu. Kuna kampuni moja ambayo iliwashika wanafunzi na vijana mapema tangu
2004/2005 kwa kuwawezesha kupiga simu bure muda wa usiku baina ya mtumiaji
mmoja wa mtandao huo na mwingine. Hata mimi wakati huo nilinunua card
yao kwa sababu iliniwezesha kuwasiliana kwa garama nafuu sana. Nimekua na
namba hiyo kwa miaka 8 sasa mbali na ukweli kuwa karibuni huduma zao zimekua
duni na za gharama ni kubwa kuliko nilipojiunga. Siku hizi wananikata fedha
hadi 5000 bila maelezo ya kueleweka. Na masiliano huwa mabaya mara nyingi. WAMENIHODHI.
Nashindwa kuwahama maana namba yangu ni muhimu sana na ninayo moja tuu.

Wakati huo,hiyo
kampuni husika ilijua kundi la wanafunzi liko katika kipindi cha MPITO. Hivyo
lilitukopesha. Sasa wengi wetu limetuhodhi  na linatupora tuu. Na hiyo
mbinu ilijenga ushawishi mkubwa kwa vijana wengi kununua kadi zao na hadi leo
wamejikuta wanakuwa watu wazima na wamebaki nazo.

Naona kampuni
nyingine zimegundua hiyo monopoly ya kampuni `niliyoitaja` hapo juu hivyo
zinajaribu kuwavuta wanafunzi na vijana zaidi.  Hii ni vita ya
mafahari,nyasi lazima ziumie.

Kwa mantiki
hii,lengo katika tangazo tajwa ni zaidi ya hilo la bahati na sibu. Ni
uthibitisho wa huo ushindani wa kutaka kuhodhi kundi la wanafunzi na
vijana kwa manufaa ya kibiashara. Nia ya kutengeneza faida hapo haijali
ujumbe/tafsiri ama ushawishi hasi unaoweza  kutokana na tangazo hilo.
Atakayeponzwa nalo,hilo ni kosa lake. Shauri yake. Hiyo ndiyo neo-liberal
ethic.

ALEX:

Mkuu nimekusoma
vizuri ila heri wangeweka slogan tu….kama zile za kata wewe, sitaki kata
wewe….!!

Ila kwenda na graphic ad na mwalimu mtu mzima kabisa amejaza maths
formulas ubaoni ila anapuuzwa mhh….its kinda extreme.

They are so many
alternative moral na ethical channels to tap the market they are targeting.

Tukiruhusu
competition za kubomoa maadili kama hizi ziendelee sipati picha itakuwaje.

Waache
hii ni wrong marketing campaign,hasa hasa wakati huu ambako maadili na elimu
vimeporomoka sana (in my opinion).

Imagine then baadaye they come forward and
donate books…..!!

—-

STEPHEN:

Tajirika na
vodacom.

ADAM:

Si tumeruhusu
FEDHA ziwe msingi wa maendeleo!

EDWIN:

Haya ndIo
matangazo yanayopotosha jamii kwa kuwafanya wanafunzi na vijana wa kitanzania
waamini kuwa ELIMU HAILIPI WALA SI UKOMBOZI KATIKA MAISHA BALI MAISHA NA
UKOMBOZI WA KWELI VIMO KATIKA BAHATI NASIBU ZINAZOTOLEWA NA MAKAMPUNI YA SIMU.
Kama taifa lazima tulinde maadili na elimu yetu tusiruhusu UBWANYENYE NA
UTAWANDAWAZI VITUHARIBIE TAIFA. Nilikuwa natafakari kuhusu tangazo hilo la
mwanafunzi akiwa darasani mwalimu anafundisha mara mwanafunzi anaibuka na
kusema kwa sauti nimeshindaaaaaaa halafu darasa zima wanampongeza na baadae
mwalimu anauliza niliishia wapi wanafunzi wanamjibu kwa kusema ulikuwa
umemaliza. Napiga picha na kuirudisha nyuma kwenye darasa letu SCIENCE 2
maarufu kama S2 pale Mwanza Secondari jijini Mwanza; nakujuliza hivi
ingekuwaje? Napata jibu kwamba huyo mwanafunzi aliyeshinda angeadhibiwa vikali
sana ikiwa ni pamoja na kufukuzwa shule.

Taswira
ninayoipata katika darasa hili LA kwenye tangazo ni kwamba mwalimu anafundisha
huku wanafunzi wanachat kwenye simu zao za viganjani ndo maana mmoja wao
aliweza kubaini kwamba ameshinda na kwa midadi isiyo ya kawaida anaruka kwa
sauti huku darasa zima likimuona mwenye bahati maishaini mwake. BINAFSI
NACHUKUA WASAHA HUU KULAHANI MATANGAZO YA AINA HII KATIKA VYOMBO VYA HABARI.

EVARISTO:

Kama kawaida
angalia hata tangazo la coca cola wakati dunia inahofu na majanga au inawaza
juu ya kitu fulani Afrika inabirudika na coke, Africa haiwazi. Na tangazo hilo
ni yaleyale tu, yapo mengi sana ya ubaguzi wa rangi,  matabaka nk . Ndipo
tulipofikia.

HILDERGADA:

Inamaanisha
watoto wadogo wanakuwa na simu na huzitumia akiwa darasani. Hii ni kweli.
Wazazi walichangamkie. Ukimuuliza mtoto atakuambia uongo-kaikota huko nje,
alikuwa akijibana ukimpa hela ya nauli akanunua sm (mpunguzie nauli ni nyingi
hela umpayo) etc. Wanafunzi wengine vibaka huibia sm watu; wengine huibia hela
wazazi wao. Ukimtuma nyama kilo 2 ananunua moja na nusi au mbili kasorobo.
Umtumacho-hupunguza ili akuibie hela (usiwatume kununua bulky items hata vijana
wakubwa, kanunue mwenyewe bajeti ya familia). Ukizubaa home-anakuchomoa hela
ukiisaka anasema hajui hajaiona kumbe ipo mfukoni kwake ili naye apate simu.
Mradi sasa dunia imeharibika. Kuharibika mpaka kampuni sa sm kujisahau kuweka
matangazo hayo. Ila shule nyingine-sm inatumika kuunganisha na video system
kufanya masomo/kufundishia. Tuchague lipi linatufaa.

ALEX:

aani huwa kila
nikiliona hili tangazo nakereka sana.

Linadhibitisha ni jinsi gani hatuko
makini katika Elimu zaidi ya kufikiria ‘kutengeneza hela’ kwa kubahatisha,mkato

Ndio
maana hata pale kiongozi fulani anapoteuliwa nchini au nje ya nchi kushika
nyadhifa fulani utasikia magazeti yanasema XX AMEULA au AMEUKATA etc…

Hii
inaonyesha jinsi gani tumeweka mbele Hela za kubahatisha na kupenda njia za
mkato.

Linapaswa kukemewa na kufutwa ikizingatiwa tunapiga kelele vijana
wanaenda shule madarasa na majengo hayatoshi ila cha kushangaza mwaka huu
kidato cha tano madarasa na mabweni ndio yamekosa wakukaa eti,hakuna wanafunzi
wanaofuzu.

KIULA:

I see! Kumbe
macho ya wanazuoni yanafanana sana! Siku mbili zilizopita hili tangazo
lilinifikirisha sana hasa pale wanafunzi wanapomjibu mwalimu kuwa
…”ulikuwa umemaliza” wakati alikatishwa kwa kelele za aliyekuwa
akishangilia kuwa ameshinda. Pengine linaakisi hali halisi iliyopo mashuleni na
namna wanafunzi wa leo wanavyoichukulia elimu.

CHAGGAMA:

Labda voda
washitakiwe kwa corrupt public morals.

Unlike
cultural/tribal values/morals or religious institutions
shule zinatengeneza coporate morals at an inclusivistic sense. Hivyo
basi Watoto humtazama mwalimu kama role model which inadvertently corrupts
public morals.

Labda mjadala
huu utawafikia waalimu/ serikali na makampuni za simu.

NAMTASHA:

Samahani naomba niulize, je nchini kunayo coalition yoyote
ambayo ingeweza kufuatilia na kukemea vitendo amabvyo vinazidi kuharibu mawazo,
mtazamo na utamaduni wa Mtanzania kwa ujumla?

http://groups.yahoo.com/group/Wanazuoni/message/19734