
KTY: Kwa mujibu wa hotuba hii ya Bajeti aliyotoa Waziri huyo, kati ya sekta/maeneo 6 “muhimu” ambayo “kwa pamoja yametengewa jumla ya shilingi bilioni 5,103.2 sawa na asilimia 64 ya bajeti yote ya mwaka 2009/10”, ni sekta ya nishati na madini tu ambayo bajeti yake ilipungua/ilipunguzwa kutoka kwenye bajeti ya mwaka jana – za zingine 5 zilizobakia ziliongezeka kama takwimu hizi na asilimia zake za ongezeko kwenye mabano zinavyoonyesha:
Elimu: Sh Bilioni 1, 743. 9 kutoka 1,430.4 (22%)
Kilimo: Sh Bilioni 666.9 kutoka 513.0 (30%)
Miundombinu: Sh Bilioni 1,096.6 kutoka 973.3 (12.7%)
Afya: Sh Bilioni 963. 0 kutoka 910.8 (5.7%)
Maji: Sh Bilioni 347.3 kutoka 231.6 (50%)
Swali: Kuna uhusiano gani kati ya maeneo haya 5 yaliyopata ongezeko na eneo la 6 la ‘nishati+’ lililopata punguzo?
Jibu: Mgawo wa Elimu, Kilimo, Miundombinu, Afya na Maji!