Tuliwahi kuambiwa ardhi na watu wanahitajika ili tuendelee. Leo tumeongezeka hadi kufikia milioni 44+. Pia tunaambiwa kuwa bado tuna ardhi nyingi ndio maana ‘inawekezwa’. Wapo wanahistoria wa uchumi wanaodai kilichofanya/kinachofanya tusiendelee kiuchumi ni mchanganyiko wa kutokuwa na nguvukazi ya kutosha (watu) ya kutumia ardhi ‘tele’ tuliyonayo n.k. Je, hili ni kweli? Nimeambatanisha makala inayochambua hilo.