TUMEPEWA:
▪︎ Nyerere Day
▪︎ Karume Day
Tunashukuru.
Sasa tunataka:
▪︎ Bibi Titi Day
Tukumbuke, Bibi Titi Mohamed alikuwa Simba Jike, mpiganaji wa Uhuru wa Taifa letu.
Bibi Titi Mohamed alichangia mengi mno, mengine tutaweka kwenye kitabu tunachoandaa juu yake.

“Waliosimama kutoka kushòto Bìti Kaijage, Biti Sheikh, Biti Mwanandege walioketi kushoto Mama Boi, Bibi Titi na Biti Farahani. Hawa walikuwa viongozi wa Umoja wa akina mama wa TANU Bukoba” (Mohamed Said, https://www.jamiiforums.com/threads/bibi-titi-mohamed-na-akina-mama-wa-bukoba-1950s.1901329/)

Hii ni orodha fupi ya mchango wa Bibi Titi kwenye harakati za kupata Uhuru wa Tanganyika, hadi ikawa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (JMT) baada ya kuungana na Zanzibar:
▪︎ Bibi Titi aliweza kuingiza wanawake kwenye harakati za kupata Uhuru.
▪︎ Bibi Titi aliongeza jimbo la Waswahili kwenye mtandao wa harakati za kupata Uhuru.
Jimbo la Waswahili lilikuwa muhimu mno kwenye harakati za ukombozi wa Taifa letu adhimu
▪︎ Bibi Titi aliweza kupita kwa matajiri wenye asili ya Kiasia, kuchangisha fedha.
Akina Baba yake  Mzee Alnoor Kassam, Karimjee Jivanjee na wengineo.
▪︎ Bibi Titi alichukua nyimbo na tenzi za Kiswahili, zikaingizwa kwenye Kaulimbiu ya mchakato wa kuhamasisha wananchi wajiingize kwenye mapambano ya Uhuru.
Mojawapo ni Hongera Mwanangu.
▪︎ Bibi Titi aliweza kutumia vikundi vya ngoma vya lele mama, vihamasishe Uhuru.
▪︎ Bibi Titi alisafiri nchi nzima, kuhamasisha wananchi wajiunge na mchakato wa Uhuru.
▪︎ Bibi Titi aliweza  kuwafikia mpaka waliopo ndani, wanawake wa makabila yote, kujiunga na mchakato wa Uhuru.
▪︎ Bibi Titi alikuwa na kipaji cha kutoa hotuba, akasikika, akaaminika.
Kwa kweli orodha ni ndefu.

Kwenye kilio cha Bibi Titi, nyumbani kwake Upanga, 2000. Mwanahabari mwandamizi Leila Sheikh akiongoza Dua ya Khitma, ya kumrehemu Simba Jike, Titi Mohamed.

Sisi tuliobahatika kumfahamu kwenye mwisho wa uhai wake, tumepata lulu na almasi kutoka kwa Bibi.
Tupewe Bibi Titi Day.

Hatimiliki

Udadisi imetumia picha kutoka kwa Leila Sheikh na Mohamed Said.