Taratibu za kuwasilisha Muswada
- Andiko bunifu litumwe kama kiambatisho kwa Microsoft Word au nukta nundu.
- Kiambatisho kiwe na jina la andiko bunifu na nyanja aliyoiandikia.
- Ukurasa wa kwanza wa andiko bunifu uwe na kichwa cha andiko bunifu na jumla ya maneno au idadi ya mashairi.
- Andiko bunifu liwe na namba kwenye kila ukurasa.
- Andiko bunifu litumie “Times New Roman” ukubwa wa herufi uwe 12 na “double spacing”.
- Mwandishi asiandike jina lake wala taarifa binafsi kwenye andiko bunifu.
- Mwandishi aweke taarifa zifuatazo kwenye barua pepe itayoambatana na mswada wake: Majina matatu, jina la uandishi (kama analo), Jinsia, namba ya simu, anuani, wasifu usiozidi maneno 150 na umri. Usiweke taarifa hizi kama kiambatisho.
- Kila mshiriki atatakiwa kusaini tamko la kuthibitisha kuwa muswada huo ni wake na haujachapishwa mahali popote ikiwemo mtandaoni na magazetini.
Pakua hapa tamko bit.ly/TAMKOTUZO - Andiko bunifu liwasilishwe kati ya Agosti 16 na Novemba 30, 2024.
- Tafadhali tuma wasilisho lako kwa “tuzonyerere@tie.go.tz”.
Vigezo Nyanja ya Ushairi
- Mshiriki awe raia wa Tanzania.
- Washindi wa 1-3 wa Tuzo hii wa miaka iliyopita hawaruhusiwi kushiriki katika tuzo kwenye nyanja yoyote ile kwa kipindi cha miaka 2 kuanzia mwaka alioshinda.
- Andiko bunifu liwe katika lugha ya Kiswahili.
- Mashairi yasipungue 50 na yasizidi 60, idadi ya beti kwenye kila shairi isizidi 15.
Pia, ikiwa muswada ni utenzi uwe utenzi mmoja tu na uwe beti kati ya 300-400. - Sehemu yoyote ya muswada isiwe imechapishwa na mchapishaji au kuchapishwa binafsi pamoja na kuchapishwa mtandaoni na magazetini au kurushwa katika vyombo vya habari na burudani au kuoneshwa jukwaani.
- Mwandishi anaruhusiwa kushiriki andiko bunifu moja tu katika nyanja atakayochagua.
- Muswada utakaoshinda tuzo nyingine hautazingatiwa.
- Miswada iliyoshika nafasi 4-10 katika tuzo ya miaka iliyopita haitaruhusiwa kushiriki. Mwandishi aliyeshika nafasi 4-10 anawezakuleta muswada mwingine.
- Andiko bunifu litakalowasilishwa liwe andiko makini lililojikita kwenye masuala muhimu ya jamii.
Vigezo Nyanja ya Tamthiliya
- Mshiriki awe raia wa Tanzania.
- Washindi wa 1-3 wa Tuzo hii wa miaka iliyopita hawaruhusiwi kushiriki katika tuzo kwenye nyanja yoyote ile kwa kipindi cha miaka 2 kuanzia mwaka alioshinda.
- Andiko bunifu liwe katika lugha ya Kiswahili.
- Sehemu yoyote ya muswada isiwe imechapishwa na mchapishaji au kuchapishwa binafsi pamoja na kuchapishwa mtandaoni na magazetini au
kurushwa katika vyombo vya habari na burudani au kuoneshwa jukwaani. - Mwandishi anaruhusiwa kushiriki andiko bunifu moja tu katika nyanja atakayochagua.
- Muswada utakaoshinda tuzo nyingine hautazingatiwa.
- Andiko bunifu litakalowasilishwa liwe andiko makini lililojikita kwenye masuala muhimu ya jamii.
- Muswada uwasilishe wazo asili la mwandishi.
- Muswada utumie vionjo vya sanaa za maonyesho za Kitanzania.
- Tamthilia ya jukwaani iwe na dakika 40 hadi 60, iwe na maonyesho yasiyozidi 6
na wahusika katika tamthiliya wasizidi 6. - Tamthilia ya runinga iwe na “episodi 13”. Kila “episodi” katika tamthiliya iwe ya muda usiozidi dakika 30.
- Tamthilia ya redio iwe na “episodi 13”. Kila episodi katika redio iwe na muda usiozidi dakika 30 na wahusika katika tamthiliya wasizidi 7.
Vigezo nyanja ya Hadithi za watoto
- Mshiriki awe raia wa Tanzania.
- Washindi wa 1-3 wa Tuzo hii wa miaka iliyopita hawaruhusiwi kushiriki katika tuzokwenye nyanja yoyote ile kwa kipindi cha miaka 2 kuanzia mwaka alioshinda.
- Andiko bunifu liwe katika lugha ya Kiswahili.
- Hadithi ya Watoto iwe kati ya maneno 250 na 1,000.
- Hadithi itakayowasilishwa ilenge watoto wa miaka 5 hadi 12.
- Muswada utakaowasilishwa ujumuishe michoro.
- Muswada wa Hadithi za Watoto utumwe kama PDF na sio word document.
- Hadithi itakayowasilishwa itumie lugha rahisi inayoeleweka.
- Sehemu yoyote ya muswada isiwe imechapishwa na mchapishaji au kuchapishwa binafsi pamoja na kuchapishwa mtandaoni au gazetini.
- Mwandishi anaruhusiwa kushiriki andiko moja tu katika nyanja atakayochagua.
- Muswada utakaoshinda tuzo nyingine hautazingatiwa.
- Miswada iliyoshika nafasi 4-10 katika tuzo ya miaka iliyopita haitarihusiwa kushiriki, hata hivyo mwandishi aliyeshika nafasi 4-10 anaweza kuleta muswada mwingine.
- Andiko bunifu litakalowasilishwa liwe andiko makini litakalojikita katika masuala muhimu ya jamii.
Leave A Comment