Unyagoni
Mwanahamisi ‘Mishy’ Singano
Basi bwana…. mapenzi yakawa mahaba, tukasema, mbona twajinyima, hatulali tukaamka, hatupiki, tukapakua, twajipa wasiwasi na wahka, kwa nini tusioane? Naammm…. Familia zikajua, hapo ndiyo utamu ulipoanza, nilipoyajua ya usungo na ya utangani….
Pirika zikaanza, posa ikakabidhiwa, haaa-madi…. Kumbe ni barua, yeye maneno yaliyoyoonyoka, “Familia ya Bwana Fulani, yatakumuoa bint yako Fulani.”Hapo ndipo nilipojua, kumbe naolewa na familia siyo ‘bwana flani’, hilo moja. Kilichonishangaza, ni kuwa, barua hiyo ilifungwa na hela, ikatiwa kwenye bahasha, bahasha ikafungwa na leso, na kukaziwa na pini zile za zamani.
Walai sijapata maana ya yakini mpaka leo hii, ila mjomba wangu mie, wakati ule, aliniambia kuwa, kwanza barua hufungwa hivyo ili kutofautisha, na barua nyingine kwa kuwa barua ya posa lazima ifunguliwe na watu wanaostahili, lakini pesa – ambazo hazirudishwi (nonrefundable), ni kulipia gharama za upofu (maana kusoma kunatia upofu ati) – nami nilicheka kama wewe. Lakini leso ni kwa ajili ya babu kujifuta jasho na machozi ya hamaki na furaha kwa kuibiwa mke wake (muolewaji) na pini ni ya kumpa bibi, kukazia mkaja wake.
Mapokezi ya posa huja na maulizo ya muolewaji, nami nikawajibu ‘are you kidding me?’ yes, nataka kuolewa…. vigelegele vikapigwa, shangwe na nderemo, thenwazee wakakaa kama kamati, kuandaa mahari…. Shughuli haikuwa ndogo, mana mie ni mixture, ya msambaa, mdigo, mbondei na mzigua…. Na ilibidi wakubaliane mfumo wa mahari yangu… Kisambaa, jamaa alitakiwa anivizie nimelala kwenye nyumba ya baba yangu na kuja kunibeba usiku wa manane – yes, kuniteka kind of, ila wangefunga mbuzi nje kuelezea aina ya utekaji na asubuhi, familia yake ingekuja na mali kujitambulisha, ‘Kughuigwa’ Kizigua.
List ya mahari lazima iwe kubwa mno kwa sababu, waoaji wana haki ya kutoa gharama walizotumia kipindi chote cha uchumba, oh yes, kama niliwahi kulala kwake na nikanywa chai, that laki moja down, kama alinihonga hela ya wigi, that laki mbili down, so at the end, inawezekana kabisa familia ya mke ndio itatakiwa iwalipe waoaji, so strategically, inabidi watoe bonge la bili, ili hata wakikata… hasa kwa binti kama mie ambaye sisomeki, stillwazee wabaki na chochote. Kwa kidogo, mahari ni security ya mwanamke, kwa hiyo, furniture za ndani kwao ni bora zaidi ili mume akifikiria kukuacha anajiuliza mara mbili kama yuko tayari kulala chini, maana utaondoka na vitanda na makochi yote, anyways… list ikatengenezwa, mahari ikajaa kurasa ya A4, jogoo, mbuzi, mche wa sabuni na kuendelea…
Utamu ukaja mimi, kukataa kulipiwa mambo ya kimila na kuuzwa… ‘the feminist in me, timbwili lake halikuwa dogo, ila mwisho wa siku nikaambiwa mahari inabidi ilipwe na haitakiwi kulipwa yote – ni amri siyo ombi! Mumeo atamalizia hiyo mahari siku atakayokuacha…I was like …. why? Bibi akaniambia, kidini hatakiwi kukuacha kabla hajamaliza mahari na kimila hatupokei mahari yote, na lengo ni kumfanya mume, afikirie ‘gharama’ ya kukuacha, nikatoa mimacho…. Nikavuta pumzi, nikauliza, je mimi nikitaka kumuacha? Nikaambiwa itanipasa nimlipe mahari yake aliyonilipia… I decided to go cheap, just in case … Ha ha ha.… anyway… hili la mahari tutaliongea next time….
Now that, nshalipiwa … haloooo! ni muda wa kuandaliwa, kwenda kumliwaza bwana… wakatafutwa masomo na manyakanga, mwali nikaingizwa unyagoni. Samahani somo yangu… nausokorotora unyago… kwa leo tu…
Bi dada nikachukuliwa kupelekwa unyagoni….nikisindikizwa na wamama, vicheko na nderemo mie moyo wapitwa kama jipu la kisigino… Kufika kwa somo, ngoma zikakazana, somo akanijia… nimefunikwa gubigubi… huku wakiimba kwa furaha na hamasa… njoo nae mwari wako njoo nae… hakuna mwari asiye na somo, njoo naye…. Mpaka katikati, kuinua kichwa nimezungukwa na manyakanga wasiopungua 50, kufa nataka kuishi nakutamani…. Nikasema courage Mishy! Sasa si wakaanza kunivua nguo moja baada ya nyengine (kikundi cha manyakanga kama watano hivi walinizunguka) wengine wakiwa busy na nyimbo, na ngoma na vigelegele…. At that time, nikuwa nusu mtu nusu marehemu…. Kutahamaki nimefungwa upande wa kanga nikawekwa chini – katikati.
Kwanza nikafundishwa salaam, kuwasalimia wale tu waliochezwa kabla yangu, nikapiga magoti, nikaweka mikono nyuma, na kuinamisha kichwa, ili wanibariki kichwani… nikatambaa na magoti kuwasalimu wote… isipokuwa wale ambao hawakuchezwa. Nikarejea katikati ya kilinge (kwa magoti), nikaa kitako, miguu nimenyoosha… kichwa nimeweka chini, umwari haswa…. by that time, I felt empty, walinivua umimi wangu.. nikabaki debe tupu.
In the middle of that…. wakakaribishwa mama na mashangazi, kuwaambia manyakanga maovu na mapungufu yangu ili manyakanga… wanifix… ule msemo wa samaki mkunje angali mbichi, it’s a lie, mie nilikunjwa nikakauka kabisa. Wakaanza kuongea…. man…. that was tough… yaani wale wazee walinisema niliyoyajua na nisiyoyajua, yaliyowaumiza na nayowakwaza, sasa sikwambii masomo walivyokuwa wanashadadia na kunisuta… and I should have said, unyago huu ulifanyika Kariakoo…. So you could imagine…. Nilichambwaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa mpaka nikapauka.
Then nikaamriwa kutambaa na magoti na kwenda kuwaomba msamaha wazee wangu ‘Wanisafie nia’ Nakumbuka Nyakanga wangu akinambia, Mishy, bila radhi za wazee wako, hata ukabinuke sarakasi za Bruce Lee huko kwa mumeo, ndoa yako haiwezi kuwa na amani…so I did… nikalia, nikatubu na kamasi zikatoka… I wished, nami wangenipa nafasi ya kusema yangu, ila mie ni mwari nilipaswa tu kusikiliza na kutubu, never the less, it was a healing moment for me…
Baada ya vilio, michambo na misamaha, manju akauchachua msondo. Kwa mujibu wao, hii ilikuwa demo kuwaonesha familia kuwa, binti yao yuko mikono salama, na nitafundwa na kufundika. Nyakanga akalala chini, nami nikalala ubavu, mikono nyuma, ushanga mdomoni, huku kiuno kikifata mdundo wa ‘mkuno wa nazi mkuno, kunia pembeni, kunia chini, kunia katikati, kunia juu.’Nikaanza kuokota mizungu.
Mmoja wa manyakanga alikuwa na fimbo mkononi, ukitegea, umechapwa nayo ya mgongo, nikajikaza kuchezesha kiuno, nikaambiwa, ‘usilete kiuno cha ndombolo, utaivunja! Kata taratibu, kifeel, kisiklizie, ringa nacho, jishaue kitandani ndiyo mahala pekee ambapo ni mali yako, own it... Hapo ndipo kazi ilipoanza…
Nilikaa unyagoni kwa siku nane – haya yalikuwa mapokezi tu.. tuonane next weekend nikujuze yaliyojiri siku ya kwanza… and mind you siku zote nane, nililazwa sakafuni kwenye mkeka… nikauliza mbona mwantesa? Nikajibiwa, “Mume aumaaa…. Kwa mateso haya… hutomtoa mumeo sadaka!” Nikahamaki…
You wrote good. Ila nikadhan ikiwa utakuwa serious na kazi Basi tumia lugha moja na ya pili I we Kama mbinu ya kifani ila kwa uchache na maeneo ambayo Ni fantastic. Ok ??