Kizazi kipya kinazidi kuingia deep katika kumuvuzisha maneno ya Kiingereza kwenye Kiswahili bila kujali kanuni za kutohoa. Ni dhahiri kuwa hali hii ndio ‘imepelekea’ ticha mmoja mdadisi aamue kutinga kortini kuinusuru jeneresheni hii ya bongo flava. Kwa mujibu wa gazeti la The Citizen la Jumatatu hii, mwalimu huyo ataishtaki Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi kwa kukataa kwa makusudi kutumia lugha ya Kiswahili kufundishia katika ngazi zote za elimu nchini Tanzania. Amenukuliwa akisema kuwa watoto wetu na taifa ‘limesafa sana’ kutokana na hilo.

Inasemekana mwalimu huyu amefanya risechi mbalimbali na kuhojiana na wadau mbalimbali kupruvu athari zilizosababishwa na kufosi madenti wafundishwe kwa lugha ya Inglishi. Pia amefanya dibeti nyingi na madenti ambao wengi wao wamekiri kuwa wanapasi pepa kwa kuwa wanakremu. Ticha huyu aliyeritaya kufundisha sekondari anasisitiza kuwa ana sapoti ya nguvu kutoka kwa Baraza la Kiswahili (BAKITA).

Aironikali, gazeti la leo la The Citizen linaripoti kuwa Jaji mkuu wa Zanzibar ameishauri Serikali ikifanye Kiswahili kuwa lugha ya mawasiliano katika korti za Visiwani. Jaji huyo amekiri kuwa waendesha mashitaka wengi ‘hawako vizuri’ katika Kiingereza. Inasemekana kuwa advaisi yake iko paraleli na vyuz za Jaji mkuu wa Tanzania. Hakika chenchezi hizi zikitokea basi ‘zitamwezesha’ ticha kuishtaki vizuri Wizara husika kuhusu suala la lugha ya kufundishia. Mdadisi anauliza, je tutakwenda kuwa witinesi kwenye kesi hiyo au tutabakia kudadisi tu?

Kwa udadisi zaidi soma makala ya ‘Can we teach what we don’t know?’ iliyohifadhiwa katika blogu hii – bado blogu ina changamoto ya kiteknolojia mambo yakiwa supa basi linki za makala hizi n.k. zitakuwa zinasetiwa humu humu ili msomaji uweze kuzibofya izili, yaani, kiurahisi.