Inasikitisha na kutisha,
hata tukiififisha
kamwe haiwezi kwisha;
yarabi atupe motisha,
moto tuweze washa;
Tuli hatuwezi pisha,
Hata wakitutapisha;
Katu haya si maisha,
Bora yalotutamanisha;
Kwanini haya yasoisha,
Japo miongo yatupisha?
Si Juma wala Aisha,
Wote kiyoro haitoisha;
Kibaya isotosha, kipi
Kwa haya maisha?
Pole walo mnazi,
Masahibu si zizi;
Tukiamua ni wazi,
Kutushinda hayawezi,
Muhimu kuweka wazi!
Walituambia juzi,
Ajali hawatoenzi;
Ahadi kama juzi,
Ajali kama enzi;
Bukoba walituasi,
Tukajua wako nasi;
Nungwi tena hasi,
Tena hamtuasi?
Si nzuri hali,
Kilio kila pahali;
Ahadi bado kali,
Si bado hatuna hali?
Ah, wacha tulie,
Wetu tujalie;
Hata tutulie,
Pemba itulie!
Majaribu yapo,
Siye pia tuwepo;
Wakuu watukerapo,
Hasira iwepo!
DBW, Leo.

