Wachapishaji wa Vitabu wa E & Dwanazindua kitabu kinachohusu haki za ardhi kwa wanawake na ubinafsishajisiku ya Alhamisi, tarehe 30 Aprili 2009, kuanzia saa 10: 30 alasiri hadi saa 12: 30 jioni. Uzinduzi huu wa wazi utafanyika katika Mkahawa wa Vitabu wa Soma. Kutakuwa na mdahalo utakaofuatiwa na mjadala wa wazi. Mdahalo utawahusisha Mwenyeketi wa Kamati Maalumu ya Ardhi na Jinsia (GLTF), Dakta Magdalena Rwebangira na Mwenyekiti wa Bodi ya Taasisi ya Utafiti wa Haki za Ardhi (LARRRI/HAKIARDHI), Dakta Ng’wanza Kamata. Katibu Mtendaji wa Agenda Participation (AP2000), Moses Kulaba, ataratibu mdahalo huu na kuwezesha mjadala utakaofuatia.

————————————————————–

E & D Publishing Vision is introducing the Book Women’s Land Rights and Privatization in Eastern Africaon Thursday, 30 April 2009 from 4:30 – 6:30 pm. The public event will take place at Soma Book Cafe. It will feature a panel discussion followed by a plenary session. The panelists will include the Chairperson of the Gender Land Task Force (GLTF), Dr. Magdalena Rwebangira and the Board Chairperson of the Land Rights Research and Resources Institute (LARRI/HAKIARDHI), Dr. Ng’wanza Kamata. Moses Kulaba, the Executive Secretary of Agenda Participation (AP2000), will moderate the panel discussion and facilitate the plenary session.