Ndugu Mwanazuoni,


Blogu ya Udadisi inakuomba/inakukaribisha ulete wasifu wako iweze kuutoa katika mfululizo wa WASIFU WA WANAZUONI (WA)TANZANIA. Huu utakuwa ni mwendelezo mpya wa PROFILING TANZANIA’S SCHOLARS IN THE DIASPORA. Tofauti ni kuwa utahusisha na waliopo Tanzania.


Ili wasifu wako utokee Udadisi tukufahamu wewe na kazi/tafiti zako, tuma vitu vitatu vifuatavyo kwa chambi78@yahoo.com: (1) Picha (2) Kiunganishi cha Chapisho na (3) Tovuti yenye wasifu.


Picha inaweza katika JPG, GIF, PNG au kiunganishi/tovuti yenye picha au Video katika Youtube, ama Vimeo. Kama chapisho halina kiunganishi unaweza kulituma ili Udadisi iliweke mtandaoni liwe na kiunganishi. Tovuti ya wasifu inaweza kuwa ya Linkedin, yako binafsi, ya chuo chako, kazini kwako na kadhalika. Unaweza pia kuwa mbunifu zaidi kwa kuwasilisha taarifa zingine.


Wasalaam,


Chambi