Ndugu Wanamabadiliko,
Nimeona ni vema nitoe ufafanuzi kuhusu suala la Kamati yangu kuiagiza bodi ya TANESCO kuondoa stahili ya ‘standby generator’ kwenye mkataba wake wa kazi.
Rationale
Shirika la Ugavi wa Umeme nchini lina jukumu la kuhakikisha kuwa nishati ya umeme inapatikana kwa wananchi wote. Mkurugenzi Mkuu wa TANESCO ndiye Mtanzania aliyepewa jukumu hilo na Taifa. Iwapo mkurugenzi mkuu wa TANESCO anawekewa stahili katika mkataba wake kwamba ‘atapewa standby generator itakayolipiwa na Shirika’ maana yake ni kwamba mgawo au kukatikakatika kwa umeme ni jambo litakalokuwepo tu. Kwamba Shirika linalopasa kuhakikisha kwamba Umeme unapatikana muda wote, Bosi wake anapewa stahili ya ‘Generator’ umeme ukikatika. Bosi huyu atajuaje machungu ya kutokuwepo Umeme? Morally this is wrong. Fundamentally this is a contradiction to CEO’s mandate.
Jambo hili ni dogo sana lakini lina maana kubwa sana. Bodi ya Wakurugenzi ya TANESCO haikupaswa kuweka stahili hii.
Kuhusu wengine, kamati ya POAC haina mamlaka ya watu wengine. Mawaziri wapo kwenye kamati ya Makamba, kwenye POAC wanaohusika ni Bodi na CEO basi. Wanaonitaka kuagiza kwingine wananipa jukumu lisilo langu.
Hata hivyo kimsingi, Waziri wa Nishati hapaswi kuwa na Jenereta nyumbani kwake, iwe ya kulipiwa na Serikali au ya kujilipia mwenyewe. This is politics at higher level – Next level kabisa. Tukubali kubadilika ndugu zangu. Haya ni mambo madogo yenye maana kubwa sana.
Kuhusiana na Tanesco kutopewa fedha. Kamati imekuwa kali sana kwa serikali. Kamati ilimwita Katibu Mkuu kuhusu suala hilo. Kamati imeagiza kwamba suala hilo limalizwe haraka iwezekanavyo.
Kamati ya POAC inajitahidi sana kuhakikisha Mashirika ya Umma yanatimiza wajibu. Tunaomba mtuunge mkono na pale ambapo mnaona tumekosea, msitubeze bali mtueleze tujirekebishe. Kejeli, kurushiana maneno na kujadili mambo juu hakutasaidia Taifa letu. Tushirikiane, tusaidiane, tukosoane ili tusonge mbele kujenga Taifa letu zuri sana.
Zitto
Kweli Zitto wewe ni kiongozi mwenye maono makubwa kwa taifa letu hili Ila, wanainchi wakawaida wanawezaje kuingilia kati swala hili? Nikweli kabisa Kama waziri mwenye dhamana umeme haukatiki nyumbani kwake hawezi kuona uchungu wa taifa kwamba mpaka leo miaka 60 bado tuna umeme wa mgao. Na hii yote nikutokana na katiba yetu ya inchi ilikua kwa ajiri ya wazungu kutunyonya waafrika haikubadirika sasa ndugu zetu weusi wenye dhamana wanaitumia katiba hiyo kujineemesha na kutunyonya hivo nguvu kubwa ielekezwe kwenye mabadiriko ya katiba ili tupate katiba mpya inayo weza kuwawajibisha viongozi wenye dhamana.