“Katika ‘Zoom na Zu’ gumzo limekuwa kuhusu umuhimu wa kuhifadhi historia, na kwanini watu waliofanyia mengi nchi zao ama hawatajwi kabisa au hata kama wanatajwa basi kwa kiwango kidogo sana. Nimezungumza na Mwanahistoria na mwandishi wa vitabu maarufu Mohamed Said akiwa Tanzania, Mwanahistoria na Blogger, Chambi Chachage akiwa Marekani, Mwandishi wa habari na Mhariri, Esther Mngodo akiwa Canada pamoja na Mtaalam wa Bioteknolojia na mkusanyaji wa kumbukumbu za wanawake tofauti, Aneth Davis akiwa jijini Dar es Salaam” –https://www.youtube.com/watch?v=7xsdbdKpycU