Na Sabatho Nyamsenda (@Sabatho7)

Rugemeleza wa Nshala
Metikisa watawala
Simama wima, sogope
Lije jua uje ‘pepo

N’kataba meuchambua
Ubovu meufichua
Umeonya waziwazi
Kuwa ni wa kibazazi

Mtetezi wa Katiba
Kwa hoja na kwa jaziba
Umesema pasi soni
Wamefanya uhaini

Bandari na uchumini
Kama moyo na mwilini
Kumkabidhi dipii
Twakaribisha tibii

Taweka pato shakani
Na uhuru kwa rehani
Tutatweza utu wetu
Na urithi wa wanetu.

Msomi nguli Havadi
Umetimiza ahadi
Megoma lamba asali
Kuzilinda rasi’mali

Ipo siku tawadia
Tuzo kukuzawadia
Ya mametu Afrika
Alo huru, sitirika.

  1. Petro July 12, 2023 at 3:17 pm

    Shahiri konki

Comments are closed.