Imetimia miaka 21 leo tangu Bibi Titi Mohamed afariki dunia. Binafsi, naisheherekea siku hii kama Siku ya Bibi Titi. Naungana na Bi Leila Sheikh kuwa kwa hakika, Bibi Titi anastahili kusheherehekewa.

Wimbo huu ni furaha yangu kuwa taifa letu la Tanzania lilipewa mwanamke shupavu kama Bibi Titi Mohamed. Jina lake na liendelee kutajwa vizazi hata vizazi kwa mchango mkubwa yeye, na wanawake wengine wa enzi zake walioutoa ili tufike hapa tulipo.