Jamhuri ya Plato: Tafsiri ya Julius Nyerere
"Alikamilisha kufanya masahihisho ya kitabu...katika hali ya maumivu makali sana Jijini London wakati akipata matibabu katika Hospitali ya St. Thomas na mauti yalipomkuta, alikuwa amemaliza. Kilichomsukuma Mwalimu kudhamiria kutafsiri kitabu hiki ilikuwa nia aliyokuwa nayo kuwa kitabu hiki kiwe kimechapishwa kabla ya uchaguzi wa mwaka 2005, ambao alihisi ungekuwa na utitiri wa wagombea....na kuwa kungetokea misukosuko mingi nchini. Alitamani sana kuuandaa umma wa Tanzania kuchagua kiongozi bora siyo bora kiongozi" - Dibaji









